Muziki
Nifundishe Mwenendo wa Nuru


194

Nifundishe Mwenendo wa Nuru

Kwa sala

1. Nifundishe mwenendo wa nuru;

Nifundishe kuomba kwa Mungu;

Nifundishe nijue mazuri;

Nifundishe kwenda nuruni.

2. Njoo mwana tujifunze wote

Kuzishika amri zake zote,

Ili turudi kwake nyumbani—

Siku zote tuwe nuruni.

3. Baba yetu twashukuru leo

Kwa mwongozo wako wa upendo.

Twakutukuza kwa nyimbo nzuri.

Ndiyo, ndiyo twaja nuruni!

Maandishi na muziki: Clara W. McMaster, 1904–1997. © 1958 IRI

Isaya 2:5

Waefeso 5:8