Muziki
Najua Bwana Aishi


67

Najua Bwana Aishi

Kwa furaha

1. Najua Bwana aishi,

Mwokozi, Mwana wa Mungu,

Aliyekishinda kifo,

Kristo, Mkombozi wangu.

2. Mwamba wangu anaishi,

Ndiye tumaini letu,

Mwangaza uongozao,

Hadi tufikie mbingu.

3. Nipe Roho wako, Bwana,

Nipate amani yako.

Nipe imani nipite

Njia irudiyo kwako.

Maandishi: Gordon B. Hinckley, 1910–2008. © 1985 IRI

Muziki: G. Homer Durham, 1911–1985. © 1985 IRI

Mafundisho na Maagano 76:22–24, 41–42

Ayubu 19:25