166
Upendo Nyumbani
Kwa hamasa
1. Kuna uzuri kote
Penye upendo;
Furaha ipo tele
Penye upendo.
Amani na neema,
Zabubujika hapa.
Muda wote ni raha
Penye upendo.
Upendo, nyumbani;
Muda wote ni raha
Penye upendo.
2. Nyumbani kuna shangwe
Penye upendo;
Hakuna chuki kamwe
Penye upendo.
Waridi zinastawi;
Dunia ni bustani,
Maisha huwa heri,
Penye upendo.
Upendo, nyumbani;
Maisha huwa heri,
Penye upendo.
3. Mbingu hutabasamu
Penye upendo;
Dunia ni karimu
Penye upendo.
Mito hutuimbia;
Angani kunang’aa.
Mungu naye apenda
Penye upendo.
Upendo, nyumbani;
Mungu naye apenda
Penye upendo.
Maandishi na muziki: John Hugh McNaughton, 1829–1891
Mahubiri 9:9