127
Twarudisha Kwako
Kwa shukurani
1. Twarudisha kwako
Baraka adhimu;
Twajua tulivyo navyo
Umetupa, Mungu.
2. Wingi wa neema,
Kama wakadamu,
Twapokea na kuleta
Milimbuko yetu.
3. Kuwapa faraja,
Kupoza taabu,
Wanyonge kuhudumia
Ndiyo kazi kuu.
4. Twaamini neno,
Japo tu dhaifu;
Kila tuwatendealo,
Twatenda kwa Yesu.
Maandishi: William Walsham How, 1823–1897
Muziki: Hajulikani, mpangilio na Lowell Mason, 1792–1872, na George J. Webb, 1803–1887
Mithali 3:9
Mathayo 25:34–40