11
Asante Mungu kwa Nabii
Kwa uchangamfu
1. Asante Mungu kwa nabii,
Kutuongoza hizi siku.
Asante kuleta injili,
Iongezayo ufahamu.
Asante kwa kila baraka,
Pia kwa ukarimu wako.
Twapenda kukutumikia
Na kuzitii amri zako.
2. Na shida zinapotuzonga,
Na kutisha amani yetu,
Matumaini hutujia,
Kwamba wokovu u karibu.
Hatuna mashaka kwa Mungu
Ni dhahiri toka zamani.
Hakika wataangamizwa
Waovu wapinga Sayuni.
3. Tutamsifu siku zote.
Rehema zake tutaimba,
Tufurahie injiliye,
Na mwangaza wenye uzima.
Ukamilifu wa milele
Watapewa waaminifu,
Wakanao injili hii
Furaha hawata fahamu.
Maandishi: William Fowler, 1830–1865
Muziki: Caroline Sheridan Norton, 1808–mnamo 1877