128
Kuna Lolote Jema Nimefanya?
Kwa uchangamfu
1. Kuna lolote jema nimefanya?
Kuna niliyemuinua?
Kuna mwenye dhiki niliyefariji?
La sivyo, nimekosa.
Niliondolea mtu vikwazo
Kwa kujitolea kwangu?
Walipata nusuri wachovu nao?
Walipoita, nilijibu?
[Chorus]
Amka, fanya zaidi
Ya kuota u mbinguni.
Tenda jema daima, utafurahia
Baraka za maadili.
2. Fursa za kazi zipo hata sasa,
Nafasi zatujia tele.
Chunga usipitwe, usihairishe,
Bali nenda kafanye.
Ni uadilifu mtu kutoa;
Upendo unathawabu.
Mtenda jema, yeye ni msaada.
Wema sio bure kwa Mungu.
[Chorus]
Amka, fanya zaidi
Ya kuota u mbinguni.
Tenda jema daima, utafurahia
Baraka za maadili.
Maandishi na muziki: Will L. Thompson, 1847–1909, yamebadilishwa
Yakobo 1:22, 27