Muziki
Nahisi Upendo


189

Nahisi Upendo

Kwa hisia

1. Nahisi upendo

Wa Bwana u karibu.

Nuru yake ipo

Kwenye kila kitu.

[Chorus]

Nitamtii Bwana

Maishani mwangu.

Nahisi upendo

Anipao Mwokozi.

2. Nahisi upendo

Unanikumbatia,

Na ninaposali,

Najawa furaha.

[Chorus]

Nitamtii Bwana

Maishani mwangu.

Nahisi upendo

Anipao Mwokozi.

3. Nahisi upendo

Anaponibariki.

Moyo ninampa

Wangu Mchungaji.

[Chorus]

Nitamtii Bwana

Maishani mwangu.

Nahisi upendo

Anipao Mwokozi.

4. Upendo wa Bwana

Nitasambaza kote.

Nitahudumia,

Baraka nipate.

[Chorus]

Nitamtii Bwana

Maishani mwangu.

Nahisi upendo

Anipao Mwokozi.

Maandishi: Ralph Rodgers Mdogo, 1936–1996; K. Newell Dayley, kuz. 1939; na Laurie Huffman, kuz. 1948

Muziki: K. Newell Dayley, kuz. 1939

© 1978, 1979 na K. Newell Dayley. Inatumika kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.

Yohana 15:10–12