Muziki
Baba Yangu


164

Baba Yangu

Kwa hamasa

1. Baba yangu, uishiye

Palipo patukufu,

Lini nitarudi kwako,

Na tena nisujudu?

Je, kwako patakatifu,

Niliishi kiroho?

Asili yangu ya kwanza,

Nililelewa kwako?

2. Kwa kusudi la pekee

Naishi duniani,

Na bila ya kumbukumbu

Ya wangu uasili;

Kuna muda nasikia

Nong’ono, “Sio kwenu,”

Na nahisi natokea

Mahali patukufu.

3. Kupitia Roho wako,

Nilikuita Baba.

Hadi kurejeshwa nuru

Sababu sikujua.

Mbinguni kuna Baba tu?

Maana haileti!

Kweli ni mantiki; kweli

Nina mama mbinguni.

4. Niiachapo dunia,

Mwili niulazapo,

Baba, Mama, mtaacha

Niwaone mliko?

Basi nikishamaliza

Kufanya kazi zote,

Ikiwa mtakubali,

Ruhusu kwenu nije.

Maandishi: Eliza R. Snow, 1804–1887

Muziki: James McGranahan, 1840–1907

Warumi 8:16–17

Matendo ya Mitume 17:28–29 (22–31)