83
Bwana Tunakuomba
Kwa sala
1. Bwana tunakuomba,
Bariki mafundisho
Na kwa kila mmoja
Yabaki mpaka mwisho.
2. Wakati wa ujana,
Tutafuata amri.
Utuongoze vyema,
Tupe nguvu tutii.
3. Baba mwenye huruma,
Tutafutapo haki,
Utujaze furaha
Tunapofanya kazi.
4. Tusamehe makosa;
Epusha vishawishi.
Ndipo tuishi vyema
Kitukufu mbinguni.
Maandishi: George Manwaring, 1854–1889
Muziki: Benjamin Milgrove, 1731–1810; umepangwa na Ebenezer Beesley, 1840–1906
Zaburi 119:33–35