Muziki
Japo Kuna Matatizo


60

Japo Kuna Matatizo

Kwa uchangamfu

1. Japo kuna matatizo,

Jikazeni kwa bidii!

Na siku ya ufufuo

Itaeneza ukweli,

Itaeneza ukweli.

2. Japo shida zatuzonga,

Punde muda si mrefu,

Kristo atakuja tena,

Na wingi wa utukufu,

Na wingi wa utukufu.

3. Msifuni Mungu kwa nyemi;

Furaha yenu idumu.

Japo bado kuna dhiki,

Amani ipo kwa Yesu,

Amani ipo kwa Yesu.

4. Japo tumedhulumiwa,

Na kuporwa na adui,

Ipo ahadi ya Bwana;

Azma yake haikomi,

Azma yake haikomi.

5. Kazi yasonga kwa kasi

Kwa matukio makuu,

Ufalme wa zama hizi

Utajaza ulimwengu,

Utajaza ulimwengu.

6. Japo mwovu atanuna,

Maneno ya manabii

Yatasimama imara;

Hakuna wa kubatili,

Hakuna wa kubatili.

7. Litukuzwe lake jina,

Atumaye watumishi

Kuambia mataifa

Habari ya ukombozi,

Habari ya ukombozi.

Maandishi: Eliza R. Snow, 1804–1887

Muziki: George Careless, 1839–1932

Mafundisho na Maagano 58:2–4

Yohana 16:33