Muziki
Mwokozi Amefufuka


112

Mwokozi Amefufuka

Kwa shangwe

1. Mwokozi amefufuka, Haleluya!

Tuseme na malaika, Haleluya!

Ushindi kwake juu, Haleluya!

Imba dunia na mbingu, Haleluya!

2. Ukombozi ameleta, Haleluya!

Na vita amevishinda, Haleluya!

Yesu hana mateso, Haleluya!

Na giza tena haliko, Haleluya!

3. Kristo tena anaishi, Haleluya!

Nguvu ya kifo i wapi? Haleluya!

Afa kutuokoa, Haleluya!

Kaburi u wapi sasa? Haleluya!

Maandishi: Charles Wesley, 1707–1788

Muziki: Hajulikani, Lyra Davidica, 1708

Mathayo 28:5–6

1 Wakorintho 15:20, 53–57