45
Twashukuru Mungu
Kwa heshima
1. Twashukuru Mungu
Kwa moyo na sauti,
Miujiza yake
Wanyonge tunakiri;
Tangu tu wachanga
Ametuongoza,
Na baraka zake
Bado anatupa.
2. Ewe Mungu wetu,
Kuwa nasi daima
Tuwe na amani,
Tuwe nayo furaha,
Utupe upendo
Na utuongoze.
Tuepushe dhambi,
Kwa nguvu tulinde.
Maandishi: Martin Rinkhart, 1586–1649; yametafsiriwa na Catherine Winkworth, 1829–1878
Muziki: Johann Crüger, 1598–1662
1 Mambo ya Nyakati 16:8–14