Muziki
Msikilize Nabii


16

Msikilize Nabii

Kwa furaha

1. Msikilize nabii

Na neno la Mungu,

Ufurahie ukweli

Uimbe kwa nguvu.

Tumeshaipata njia

Ya wale wa mwanzo.

Nabii mpya katumwa

Kurejesha neno.

2. Giza nene lilitanda

Kote duniani,

Bwana amelifukuza,

Mungu anaishi.

Kupitia njama mbovu

Zikawapotosha,

Lakini Watakatifu

Wamepata njia.

3. Hawategemei mtu

Na yake mikono.

Wamkataao Yesu,

Laana ni yao.

Anasema Mkombozi,

“Nifuate, njoo,

Neno langu ulitii

Hata mpaka mwisho”.

4. Sikia neno la kweli

Safi vyanzo vyake.

Amri zake uzitii

Hadi uteule,

Na uvalishwe na Mungu

Taji la milele,

Utapata utukufu,

Urithi wa shangwe.

Maandishi: Joseph S. Murdock, 1822–1899. Ubeti wa nne, Bruce R. McConkie, 1915–1985. © 1985 IRI

Muziki: Joseph J. Daynes, 1851–1920

Joseph Smith—Historia ya 1:14–17

Mafundisho na Maagano 21:4–7