5
Juu ya Mlima
Kwa uthabiti
1. Juu ya mlima
Bendera ilipo,
Mataifa, ona;
Ipeperukavyo.
Ni katika Desereti,
Kwenye mlima Sayuni!
2. Mungu akumbuka
Ahadi za kale,
Juu ya mlima
Kweli zifunguke!
Mwanga wake kivutio
Kwa wote siku za mwisho.
3. Nyumba itajengwa,
Yenye utukufu,
Semi zitakuwa
Kutoka kwa watu:
Twende kwake tujifunze,
Na tutii amri zake.
4. Huko tutafunzwa
Sheria za kweli,
Na zitatawala
Kote duniani.
Tufuate njia zake,
Ili sote tuokoke.
Maandishi: Joel H. Johnson, 1802–1882
Muziki: Ebenezer Beesley, 1840–1906
Isaya 2:2–3
Isaya 5:26