Muziki
Nyumbani ni Mbinguni


168

Nyumbani ni Mbinguni

Kwa uchangamfu

1. Nyumbani ni mbinguni,

Pakiwa na pendo,

Huleta shangwe nyingi,

Baraka za Kristo—

Amani na hisani,

Usalama, ulinzi—

Hufanya nyumbani kuwa

Kama mbinguni.

2. Familia pamoja,

Huwa na amani,

Kutumiwa na Mungu,

Twakua nuruni.

Wazazi hufundisha,

Watoto hufuata,

Kupafikia mbinguni,

Tutapo kuwa.

3. Kusali kila siku,

Tutahisi pendo,

Kusoma neno lake,

Twastawisha moyo,

Kwa nyimbo tutaomba,

“Utuonyeshe, Baba,

Njia ya kufika kwako,

Tutapo kuwa.”

Maandishi: Carolyn Hamilton Klopfer, kuz. 1936. © 1985 IRI

Muziki: W. Herbert Klopfer, kuz. 1936. © 1985 IRI

Waefeso 6:1–4

Mosia 4:13–15