186
Nawaza Ajapo Tena
Kwa unyenyekevu
1. Nawaza ajapo tena,
Mbingu zitaimba?
Je, itatanda theluji,
Ardhi kuchipua?
Nyota ile itang’ara
Zaidi ya zote?
Hakutakuwa usiku?
Watahama ndege?
Atawaita watoto
Wakae gotini,
Maana alitamka,
“Waache wawe nami.”
2. Nawaza ajapo tena,
Nitakuwa pale
Kumtazama usoni
Na kusali naye?
Nitafanya apendavyo
Niwe nuru yake,
Ili wakinitazama
Watu wamjue.
Na ijapo siku hiyo,
Ataniambia,
“Umetumikia vyema;
Baki kwangu daima.”
Maandishi na muziki: Mirla Greenwood Thayne, 1907–1997
© 1952 na Mirla Greenwood Thayne, Provo, Utah. Imefanywa upya 1980. Unatumika kwa ruhusa. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.
Mathayo 16:27
Mathayo 19:13–15