169
Dada wa Sayuni
Wanawake
Kwa uthabiti
1. Dada wa Sayuni, tushirikiane
Baraka za Mungu kuzitafuta.
Kwa nguvu tuujenge ufalme wake,
Kwa wale wanyonge tuwe faraja.
2. Tumepewa ujumbe wa malaika,
Na twajivunia kipawa hiki:
Tufanye vyote vya utu kwa pamoja
Kwa jina la huruma tubariki.
3. Azima na wito wetu ni mpana,
Kazi za kiroho tutekeleze.
Ni Roho tu atakayetufundisha
Tupate hekima tufanikiwe.
Maandishi: Emily H. Woodmansee, 1836–1906
Muziki: Janice Kapp Perry, kuz. 1938. © 1985 IRI
Wagalatia 6:2, 9–10