Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 132


Sehemu ya 132

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Nauvoo, Illinois, 12 Julai 1843, juu ya agano jipya na lisilo la mwisho, pamoja na umilele wa agano la ndoa na kanuni ya ndoa ya wake wengi. Ingawa ufunuo uliandikwa katika mwaka 1843, ushahidi unaonyesha kwamba baadhi ya kanuni zilizomo ndani ya ufunuo huu zilikuwa zimejulikana kwa nabii mapema tangu mwaka 1831. Tazama Tamko Rasmi 1.

1–6, Kuinuliwa kunapatikana kupitia agano jipya na lisilo na mwisho; 7–14, Masharti na taratibu za agano hilo yaelezwa; 15–20, Ndoa ya selestia na kuendelea kwa kundi la familia kunawawezesha wanadamu kuwa miungu; 21–25, Njia nyembamba na iliyosonga huongoza kwenye uzawa wa milele; 26–27, Sheria yatolewa juu ya kumkufuru Roho Mtakatifu; 28–39, Ahadi ya kuongezeka milele na kuinuliwa zimefanywa kwa manabii na Watakatifu katika nyakati zote; 40–47, Joseph Smith amepewa uwezo wa kufunga na kutia muhuri duniani na mbinguni; 48–50, Bwana anafunga juu yake kuinuliwa kwake; 51–57, Emma Smith anashauriwa kuwa mwaminifu na mkweli; 58–66, Sheria zinazo tawala ndoa ya wake wengi zinawekwa.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwako wewe mtumishi wangu Joseph, kwamba kwa kadiri ulivyoniomba kutaka kujua na kufahamu katika nini Mimi, Bwana, niliwahesabia haki watumishi wangu Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, na pia Musa, Daudi na Sulemani, watumishi wangu, juu ya kanuni na mafundisho ya wao kuwa na awake wengi na vimada—

2 Tazama, na lo, Mimi ndimi Bwana Mungu wako, nami nitakujibu juu ya jambo hili.

3 Kwa hiyo, autayarishe moyo wako kupokea na kutii maelekezo ambayo ni karibu kuyatoa kwako; kwa maana wale wote ambao sheria hii ilifunuliwa kwao lazima waitii vile vile.

4 Kwa maana tazama, ninalifunua kwako aagano jipya na lisilo na mwisho; na kama hamkutii agano hilo, basi bmtahukumiwa; kwa maana hakuna mtu awezaye ckulikataa agano hili na kuruhusiwa kuingia katika utukufu wangu.

5 Kwani wote watakaopata abaraka kutoka kwangu wataitii bsheria iliyowekwa kwa ajili ya baraka hiyo, na masharti yake, kama yalivyowekwa tangu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu.

6 Na kuhusiana na aagano jipya na lisilo na mwisho, liliwekwa kwa ajili ya utimilifu wa butukufu wangu; na yule aupokeaye utimilifu wake lazima atii sheria, vinginevyo atahukumiwa, asema Bwana Mungu.

7 Na amini ninawaambia, kwamba amasharti ya sheria hii ni haya: Maagano yote, mikataba, mapatano, ahadi, bviapo, nadhiri, utendaji, mahusiano, ushirika, au matarajio, ambayo hayakufanyika na kuingizwa ndani na ckufungwa na yule dRoho Mtakatifu wa ahadi, na yule aliyepakwa mafuta, kwa muda na vile vile kwa milele yote, na lililo takatifu zaidi, kwa eufunuo na amri kwa njia ya mpakwa mafuta wangu, ambaye nimemteua juu ya dunia ili kushikilia uwezo huu (nami nimemteua mtumishi wangu Joseph kushikilia uwezo huu katika siku za mwisho, na hakuna mwingine isipokuwa mmoja tu juu ya dunia kwa wakati mmoja ambaye juu yake uwezo huu na ffunguo za ukuhani huu hutunukiwa), maagano hayo hayataleta matokeo yanayofaa, uwezo, au nguvu katika ufufuko na baada ya ufufuko kutoka kwa wafu; kwani mikataba yote ile isiyofanywa kwa madhumuni haya inakoma watu wanapokufa.

8 Tazama, nyumba yangu ni nyumba ya utaratibu, asema Bwana Mungu, na siyo nyumba ya vurugu.

9 Je, nitakubali amatoleo, asema Bwana, ambayo hayakufanyika katika jina langu?

10 Au je, nitakipokea mikononi mwako kile ambacho asikukiagiza?

11 Na je, nitakuagiza wewe, asema Bwana, isipokuwa iwe kwa sheria, hata kama vile Mimi na Baba yangu atulivyowaagiza, kabla ya ulimwengu kuwako?

12 Mimi ndimi Bwana Mungu wako; na ninatoa kwako amri hii—kwamba mtu ahaji kwa Baba ila kwa njia ya mimi au kwa neno langu, ambalo ni sheria yangu, asema Bwana.

13 Na kila kitu kilichoko ulimwenguni, kama kimewekwa na wanadamu, na enzi, au himaya, au nguvu, au vitu vyenye kujulikana, chochote kitakacho kuwa, ambacho hakikuwekwa na Mimi au kwa neno langu, asema Bwana, kitatupwa chini, na ahakitabaki baada ya wanadamu kufariki, wala katika ufufuko au baada ya ufufuko, asema Bwana Mungu wenu.

14 Kwani vitu vyote vitakavyosalia vitakuwa vimewekwa na Mimi; na vitu vyovyote ambavyo havikuwekwa na Mimi vitatikiswa na kuangamizwa.

15 Kwa hiyo, kama mtu aataoa mke ulimwenguni, na hamwoi mke kwa njia ya Mimi wala kwa njia ya neno langu, na akaagana naye ilimradi wako ulimwenguni na mke pamoja naye, agano lao na ndoa yao haitakuwa na nguvu wao wakifa, na wao wakiwa nje ya ulimwengu; kwa hiyo, wao hawafungwi na sheria yoyote wakati wakiwa nje ya ulimwengu.

16 Kwa hiyo, wakati wakiwa nje ya ulimwengu wao hawaoi wala ahawaolewi; bali huwa bmalaika waliowekwa mbinguni, malaika ambao ni watumishi wahudumu, ili kuwahudumia wale wenye kustahili utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana.

17 Kwa kuwa malaika hawa hawakutii sheria yangu; kwa sababu hiyo, hawawezi kuongezeka, bali kubaki wametengana mmoja mmoja, pasipo kuinuliwa, katika hali yao ya kuokolewa, milele yote; na kutoka hapo na kuendelea wao siyo miungu, bali malaika wa Mungu milele na milele.

18 Na tena, amini ninawaambia, kama mtu ataoa mke, na kufanya agano pamoja naye kwa muda na kwa milele yote, kama agano hilo halijafanywa kwa njia yangu au kwa njia ya neno langu, ambalo ndilo sheria yangu, na kufungwa na Roho Mtakatifu wa ahadi, kupitia kwake yeye niliyempaka mafuta na kumteua kwa uwezo huu, kwa sababu hiyo, siyo halali wala haitakuwa na nguvu wawapo nje ya ulimwengu, kwa sababu hawakuunganishwa na Mimi, asema Bwana, wala kwa neno langu; wawapo nje ya ulimwengu haliwezi kupokelewa huko, kwa sababu ya malaika na miungu waliowekwa huko, ambao hawataweza kuwapita; kwa hiyo, hawawezi kurithi utukufu wangu; kwa maana nyumba yangu ni nyumba ya utaratibu, asema Bwana Mungu.

19 Na tena, amini ninawaambia, kama mtu ataoa mke kwa njia ya neno langu, ambalo ndilo sheria yangu, na kwa aagano jipya na lisilo na mwisho, na bikafungwa kwao na Roho Mtakatifu wa cahadi, na yeye aliyepakwa mafuta, na yeye niliyempa uwezo huu na dfunguo za ukuhani huu; na itasemwa kwao—Mtafufuka katika ufufuko wa kwanza; na kama itakuwa baada ya ufufuko wa kwanza, katika ufufuko unaofuata; na mtarithi eenzi, falme, himaya, na nguvu, utawala kwa marefu na vina vyote—ndipo itaandikwa katika fKitabu cha Uzima cha Mwanakondoo, ikiwa hataua, ambako ni kumwaga damu isiyo na hatia, na kama watatii katika agano langu, na hawakuua ambako ni kumwaga damu isiyo na hatia, itafanyika kwao katika mambo yote ambayo mtumishi wangu ameyaweka juu yao, kwa muda, na kwa milele yote; na yatakuwa na nguvu kamili wakati wakiwa nje ya ulimwengu; nao watawapita malaika, na miungu, ambao wamewekwa huko, kwa gkuinuliwa kwao na utukufu wao katika mambo yote, kama ilivyofungwa juu ya vichwa vyao, utukufu ambao utakuwa mkamilifu na kuendelea kwa vizazi milele na milele.

20 Kisha wao watakuwa miungu, kwa sababu hawana mwisho; kwa hiyo wao watakuwa tangu milele hadi milele, kwa sababu wanaendelea; kisha wao watakuwa juu ya vyote, kwa sababu vitu vyote vipo chini yao. Kisha watakuwa amiungu, kwa sababu wana buwezo wote, na malaika watakuwa chini yao.

21 Amini, amini, ninawaambia, isipokuwa mmetii asheria yangu, hamwezi kuufikia utukufu huu.

22 Kwa maana mlango ni amwembamba, na bnjia imesonga iongozayo kwenye kuinuliwa na mwendelezo wa cuzazi, nao waionayo ni wachache, kwa sababu hamnipokei Mimi ulimwenguni wala hamnijui.

23 Lakini kama mtanipokea Mimi ulimwenguni, basi mtanijua, nanyi mtapokea kuinuliwa kwenu; ili amahali nilipo nanyi muwepo pia.

24 Huu ndiyo auzawa wa milele—kumjua Mungu wa pekee mwenye hekima na kweli, na Yesu Kristo, baliyemtuma. Mimi ndiye. Kwa hiyo ipokeeni, sheria yangu.

25 Mlango ni ampana, na njia ni pana iongozayo bmautini; nao ni wengi waingiao kwa mlango huo, kwa sababu chawanipokei Mimi, wala hawakai katika sheria yangu.

26 Amini, amini, ninawaambia, kama mtu ataoa mke kulingana na neno langu, nao wakafungwa na aRoho Mtakatifu wa ahadi, kulingana na yale niliyoyaweka, na kama mume au mke akitenda dhambi yoyote au kuvunja agano jipya na lisilo na mwisho, na aina zote za kufuru, na kama bhawakuua ambako ni kumwaga damu isiyo na hatia, bado wataamka katika ufufuko wa kwanza, na kuingia katika kuinuliwa kwao; lakini wataangamizwa katika mwili, na cwatatolewa kwa karamu ya dShetani hadi siku ya ukombozi, asema Bwana Mungu.

27 aKufuru dhidi ya Roho Mtakatifu, ambayo bhaitasamehewa ulimwenguni wala nje ya ulimwengu, inajumuisha katika mauaji yenu ambako ndiko kumwaga damu isiyo na hatia, na kukubali kifo changu, baada ya kupokea agano langu jipya na lisilo na mwisho, asema Bwana Mungu; na yule asiyetii sheria hii kamwe hawezi kuingia katika utukufu wangu, bali catalaaniwa, asema Bwana.

28 Mimi ndimi Bwana Mungu wenu, na nitawapa sheria ya Ukuhani wangu Mtakatifu, kama ilivyowekwa na Mimi na Baba yangu kabla ya ulimwengu kuwako.

29 aIbrahimu alipokea mambo yote, yoyote aliyapokea, kwa ufunuo na amri, kwa neno langu, asema Bwana, naye ameingia katika kuinuliwa kwake, na ameketi juu ya kiti chake cha enzi.

30 Ibrahimu alipokea aahadi juu ya uzao wake, na juu ya tunda la viuno vyake—ambako katika bviuno vyake ninyi mmetoka, kama, mtumishi wangu Joseph—ambayo ilipaswa kuendelea ilimradi wao walikuwepo duniani; na juu ya Ibrahimu na uzao wake, nje ya ulimwengu wanapaswa kuendelea; kote ulimwenguni na nje ya ulimwengu yapaswa waendelee kama vile cnyota zisizoweza kuhesabika; au, kama ungeliambiwa kuhesabu mchanga wa pwani ya bahari usingeliweza kuuhesabu.

31 Ahadi hii ni yenu pia, kwa sababu ninyi ni wa aIbrahimu, na ahadi ilifanywa kwa Ibrahimu; na kwa sheria hii kazi ya Baba yangu inaendelea, ambamo hujitukuza yeye mwenyewe.

32 Enendeni, kwa hiyo, na mkazifanye akazi za Ibrahimu; ingieni katika sheria yangu nanyi mtaokolewa.

33 Lakini kama hamtaingia katika sheria yangu hamuwezi kupata ahadi za Baba yangu, ambazo alizifanya kwa Ibrahimu.

34 Mungu aalimwamuru Ibrahimu, na bSara akamtoa cHajiri kwa Ibrahimu kuwa mke. Na ni kwa nini Sara alifanya hivyo? Kwa sababu hii ilikuwa sheria; na kutoka kwa Hajiri wamechipuka watu wengi. Hii, kwa hiyo, ilikuwa ni kutimiza, miongoni mwa mambo mengine, ahadi ile.

35 Je, Ibrahimu, kwa hiyo, alikuwa na hatia? Amini ninawaambia, Hapana; kwa maana Mimi, Bwana, aniliamuru hilo.

36 aIbrahimu aliamriwa kumtoa mwanawe bIsaka; hata hivyo, iliandikwa: cUsiue. Ibrahimu, hata hivyo, hakukataa, na ilihesabiwa kwake kuwa ni dhaki.

37 Ibrahimu aliwapokea avimada, nao wakamzalia watoto; na ilihesabiwa kwake kuwa ni haki, kwa sababu walitolewa kwake, naye alitii sheria yangu; kama vile Isaka pia na bYakobo hawakufanya kitu kingine chochote isipokuwa kile walichoamriwa; na kwa sababu hawakufanya kitu kingine zaidi ya kile walichoamriwa, wao wameingia katika ckuinuliwa kwao, kulingana na ahadi, na wamekaa juu ya viti vyao vya enzi, na wao siyo malaika bali ni miungu.

38 aDaudi pia aliwapokea bwake wengi na vimada, na pia Suleimani na Musa watumishi wangu, na pia wengine wengi wa watumishi wangu, tangu mwanzo wa uumbaji hadi sasa; na hawakufanya dhambi katika lolote isipokuwa katika mambo yale ambayo hawakuyapata kutoka kwangu.

39 Wake na vimada wa Daudi aaliopewa kutoka kwangu, kwa mkono wa Nathani, mtumishi wangu, na manabii wengine waliokuwa na bfunguo za uwezo huu; na katika mambo haya hakunitendea dhambi yoyote isipokuwa katika shauri la cUria na mke wake; na, kwa sababu hiyo ameanguka katika kuinuliwa kwake, na amepokea sehemu yake; naye hatawarithi nje ya ulimwengu, kwa kuwa dnimewatoa kwa mwingine, asema Bwana.

40 Mimi ndimi Bwana Mungu wako, na nimekupa wewe, mtumishi wangu Joseph, nafasi yenye mamlaka, na aurejeshe mambo yote. Omba utakacho, nawe utapewa kulingana na neno langu.

41 Na kwa kuwa umeuliza juu ya uzinzi, amini, amini, ninawaambia, kama mtu atampokea mke katika agano jipya na lisilo na mwisho, na kama mke atakuwa na mwanaume mwingine, na ambaye hakupewa nami kwa mpako mtakatifu wa mafuta, mwanamke huyo amezini na ataangamizwa.

42 Kama mwanamke huyo hatakuwa katika agano jipya na lisilo na mwisho, naye atakutwa na mwanaume mwingine, atakuwa aamezini.

43 Na kama mume wake atakuwa na mwanamke mwingine, naye mume yuko chini ya anadhiri, yeye amevunja nadhiri yake na atakuwa amezini.

44 Na kama mke hajafanya uzinzi, bali hana hatia na kwamba hajavunja nadhiri yake, naye anajua hilo, na mimi nikakufunulia wewe, mtumishi wangu Joseph, basi wewe utakuwa na uwezo, kwa uwezo wa Ukuhani wangu Mtakatifu, kumchukua mwanamke huyo na kumpa yeye ambaye hajazini ila amekuwa amwaminifu; kwa maana yeye atafanywa kuwa mtalawa juu ya mengi.

45 Kwa maana nimeweka juu yako afunguo na uwezo wa ukuhani, ambamo ndani yake bnitarejesha mambo yote, na nitayajulisha kwako mambo yote kwa wakati wake.

46 Na amini, amini, ninakuambia, kwamba lolote autakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, katika jina langu na kwa neno langu, asema Bwana, litakuwa limefungwa milele mbinguni; na dhambi zozote butakazozisamehe duniani zitakuwa zimesamehewa milele mbinguni; na dhambi zozote mtakazo ziacha pasipo msamaha duniani zitakuwa hazina msamaha mbinguni.

47 Na tena, amini ninakuambia, yeyote utakayembariki nitambariki, na yeyote utakaye mlaani anitamlaani, asema Bwana; kwa maana Mimi, Bwana, ndiye Mungu wako.

48 Na tena, amini ninakuambia, mtumishi wangu Joseph, kwamba utakalotoa duniani, na kwa yeyote utakayempa lolote duniani, kwa neno langu na kulingana na sheria yangu, litajiliwa na baraka na siyo laana, na pamoja na uwezo wangu, asema Bwana, nalo halitakuwa na hukumu duniani na mbinguni.

49 Kwa maana Mimi ndimi Bwana Mungu wako, nami nitakuwa pamoja nawe hata amwisho wa ulimwengu, na milele yote; kwa kuwa amini ninatia bmuhuri juu ya ckuinuliwa kwako, na kutengeneza kiti cha enzi kwa ajili yako katika ufalme wa Baba yangu, pamoja na Ibrahimu dbaba yako.

50 Tazama, nimeona adhabihu zako, nami nitakusamehe dhambi zako zote; nimeona dhabihu zako katika utii kwa kile nilichokuambia. Kwa hiyo, nenda zako, nami nitakufanyia mlango wa kutorokea, kama vile bnilivyokubali matoleo ya Ibrahimu ya mwanawe Isaka.

51 Amini, ninakuambia: Amri ninampa mjakazi wangu, Emma Smith, mke wako, ambaye nimekupa, kwamba ajizuie na asipokee kile ambacho nilikuamuru kumpa yeye; kwa kuwa nilifanya vile, asema Bwana, ili kuwajaribu ninyi nyote, kama vile nilivyomjaribu Ibrahimu, na ili nipate kutaka matoleo yangu kutoka mikononi mwenu, kwa agano na dhabihu.

52 Na acha mjakazi wangu, aEmma Smith, awapokee wale wote ambao nimempa mtumishi wangu Joseph, na ambao ni wema na wasafi mbele zangu; na wale ambao siyo safi, na wamesema kwamba wao ni wasafi, wataangamizwa, asema Bwana Mungu.

53 Kwa maana Mimi ndimi Bwana Mungu wako, nanyi mtatii sauti yangu; na ninamweka mtumishi wangu Joseph, kwamba atakuwa mtawala juu ya mambo mengi; kwa maana yeye amekuwa amwaminifu juu ya mambo machache, na kutoka sasa na kuendelea nitamuimarisha.

54 Na ninamwamuru mjakazi wangu, Emma Smith, kumtii na kuambatana na mtumishi wangu Joseph, na siyo mwingine. Lakini kama hatatii amri hii ataangamizwa, asema Bwana; kwa maana Mimi ndimi Bwana Mungu wako, nami nitamwangamiza yeye kama hatatii katika sheria yangu.

55 Lakini kama hatatii amri hii, basi mtumishi wangu Joseph atafanya mambo yote kwa ajili yake, hata kama vile alivyosema; nami nitambariki yeye na kumzidisha na kumpa yeye amara mia katika ulimwengu huu, mamia ya baba na mama, kaka na dada, nyumba na ardhi, wake na watoto, na mataji ya bvizazi vya milele katika ulimwengu wa milele.

56 Na tena, amini ninasema, acha mjakazi wangu aamsamehe mtumishi wangu Joseph makosa yake; na ndipo yeye naye atasamehewa makosa yake, ambayo amenikosea Mimi; na Mimi, Bwana Mungu wako, nitambariki, na kumzidisha, na kuufanya moyo wake ufurahi.

57 Na tena, ninasema, na mtumishi wangu Joseph asitoe mali yake mikononi mwake, asije adui akaja na kumwangamiza; kwani Shetani aanatafuta kumwangamiza; kwa maana Mimi ndimi Bwana Mungu wako, na yeye ni mtumishi wangu; na tazama, na lo, Mimi niko pamoja naye, kama nilivyokuwa pamoja na Ibrahimu, baba yako, hata kwenye bkuinuliwa kwake na utukufu wake.

58 Sasa, kuhusu sheria ya aukuhani, kuna mambo mengi yanayohusiana nayo.

59 Amini, kama mtu ameitwa na Baba yangu, kama ilivyokuwa kwa aHaruni, kwa sauti yangu mwenyewe, na kwa sauti ya yule aliyenituma, nami nikampa yeye endaomenti ya bfunguo za uwezo wa ukuhani huu, kama atafanya lolote katika jina langu, na kulingana na sheria yangu na kwa neno langu, hatafanya dhambi, nami nitamhesabia haki.

60 Msiache mtu yeyote, kwa hiyo, amshambulie mtumishi wangu Joseph; kwa maana Mimi nitamhesabia haki yeye; kwa maana atafanya dhabihu ambayo ninaitaka kutoka kwake kwa ajili ya uvunjaji wake wa sheria, asema Bwana Mungu wenu.

61 Na tena, kuhusu sheria ya ukuhani—kama mtu yeyote atamposa abikira, na kutamani kuposa bmwingine, na wa kwanza akatoa idhini yake, na kama atamposa yule wa pili, nao ni mabikira, nao hawakuweka nadhiri kwa mwanaume mwingine, huyo anahesabiwa haki; hawezi kufanya uzinzi kwa maana wametolewa kwake; kwa kuwa hawezi kufanya uzinzi kwa kile kilicho chake ambacho si cha mwingine yeyote.

62 Na kama anao mabikira kumi aliopewa kwa sheria hii, hawezi kufanya uzinzi, kwani ni mali yake; nao wametolewa kwake; kwa hiyo yeye anahesabiwa haki.

63 Lakini kama mmoja au yeyote wa mabikira hao kumi, baada ya kuposwa, atakuwa na mwanaume mwingine, atakuwa amezini, naye ataangamizwa; kwa maana wao wametolewa kwake ili akuongezeka na kuijaza nchi, kulingana na amri yangu, na kutimiza ahadi iliyotolewa na Baba yangu kabla ya kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu, na kwa ajili ya kuinuliwa kwao katika dunia za milele, ili wapate kuzaa roho za wanadamu; kwani humo ndimo bkazi ya Baba yangu huendelezwa, ili apate kutukuzwa.

64 Na tena, amini, amini, ninawaambia, kama mtu yeyote aliye na mke, mtu mwenye kushikilia funguo za uwezo huu, na humfundisha sheria za ukuhani wangu, kuhusu mambo haya, halafu akaamini na amhudumie, la sivyo ataangamizwa, asema Bwana Mungu wenu; kwa maana nitamwangamiza; kwa kuwa nitalitukuza jina langu juu ya wale wote waipokeao na kutii sheria yangu.

65 Kwa hiyo, itakuwa haki kwangu, kama hataipokea sheria hii, kwa yeye kupokea mambo yoyote yale Mimi, Bwana Mungu wake, nitakayompa, kwa sababu yeye mke haamini na hamhudumii kulingana na neno langu; na ndipo yeye mke huwa mvunjaji wa sheria; na yeye mume anasamehewa kutokana na sheria ya Sara, ambaye alimhudumia Ibrahimu kulingana na sheria wakati nilipomwamuru Ibrahimu kumchukua Hajiri kuwa mke.

66 Na sasa, kuhusu sheria hii, amini, amini, ninakuambia wewe, nitakufunulia zaidi, baadaye; kwa hiyo, hii inatosha kwa sasa. Tazama, Mimi ni Alfa na Omega. Amina.