Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 133


Sehemu ya 133

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Hiram, Ohio, 3 Novemba 1831. Akiandika dibaji ya ufunuo huu Historia ya Joseph Smith inasema, “Kwa wakati huu palikuwa na mambo mengi ambayo Wazee walitaka kujua kuhusiana na kuhubiriwa kwa Injili kwa wakazi wa dunia, na juu ya kukusanyika; na ili kuenenda katika nuru ya kweli, na kufundishwa kutoka juu, mnamo 3 Novemba 1831, mimi nilimwomba Bwana na kupokea ufunuo muhimu ufuatao.” Sehemu hii kwanza iliongezwa kwenye kitabu cha Mafundisho na Maagano kama kiambatisho, na mwishowe ikapewa namba kama sehemu.

1–6, Watakatifu wanaamriwa kujitayarisha kwa ajili ya Ujio wa Pili; 7–16, Watu wote wanaamriwa kuikimbia Babilonia, na kuja Sayuni, na kujiandaa kwa ajili ya siku ile iliyo kuu ya Bwana; 17–35, Yeye atasimama juu ya Mlima Sayuni, mabara yatakuwa nchi moja, na makabila yaliyopotea ya Israeli yatarudi; 36–40, Injili ilirejeshwa kupitia Joseph Smith ili kuhubiriwa katika ulimwengu wote; 41–51, Bwana atashuka kulipiza kisasi kwa waovu; 52–56, Utakuwa mwaka wa wakombolewa Wake; 57–74, Injili itapelekwa ili kuwaokoa Watakatifu na kwa ajili ya angamizo la waovu.

1 Sikilizeni, Enyi watu wa kanisa langu, asema Bwana Mungu wenu, na sikieni neno la Bwana juu yenu—

2 Bwana ambaye aatakuja ghafla katika hekalu lake; Bwana ambaye atashuka juu ya ulimwengu wa laana ili bkuhukumu; ndiyo, juu ya mataifa yote yenye kumsahau Mungu, na juu ya wote wasio cha Mungu walio miongoni mwenu.

3 Kwani atauweka awazi mkono wake mtakatifu machoni pa mataifa yote, na miisho yote ya dunia yatauona bwokovu wa Mungu wao.

4 Kwa hiyo jitengenezeeni, jitengenezeeni, Enyi watu wangu; jitakaseni ninyi wenyewe; kusanyikeni pamoja, Enyi watu wa kanisa langu, juu ya nchi ya Sayuni, ninyi nyote ambao hamkuamriwa kukaa.

5 Tokeni katika aBabilonia. Kuweni bsafi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.

6 Kuweni na makusanyiko yenu ya kiroho, na amsemezane ninyi kwa ninyi mara kwa mara. Na acheni kila mtu alilingane jina la Bwana.

7 Ndiyo, amini ninawaambia tena, wakati umewadia ambapo sauti ya Bwana ipo kwenu ninyi: Tokeni Babilonia; ajikusanyeni kutoka miongoni mwa mataifa, kutoka pepo bnne, kutoka kona moja ya mbingu hadi nyingine.

8 aWapelekeni wazee wa kanisa langu kwa mataifa yaliyo mbali; kwenye bvisiwa vya bahari; wapelekeni kwenye nchi za kigeni; yasihini mataifa yote, kwanza juu ya cWayunani, na halafu juu ya dWayahudi.

9 Na tazama, na lo, hiki kitakuwa kilio chao, na sauti ya Bwana kwa watu wote: Enendeni nchi ya Sayuni, ili mipaka ya watu wangu ipate kupanuka, na ili avigingi vyake vipate kuimarishwa, na ili bSayuni ipate kuenea hata maeneo yaliyo karibu.

10 Ndiyo, acheni kilio kiendelee miongoni mwa watu wote: Amkeni na simameni na kwenda kumlaki aBwana harusi; tazama na lo, Bwana harusi yu aja; tokeni mwende kumlaki. Jiwekeni tayari kwa ajili ya bsiku ile iliyo kuu ya Bwana.

11 aKesheni, kwa sababu bhamjui siku wala saa.

12 Kwa hiyo, waacheni wao, walio amiongoni mwa Wayunani wakimbilie bSayuni.

13 Na acha walio wa aYuda wakimbilie bYerusalemu, katika cmilima ya dnyumba ya Bwana.

14 Tokeni miongoni mwa mataifa, hata kutoka Babilonia, kutoka katikati ya uovu, ambao ni Babeli ya kiroho.

15 Lakini amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, acheni kukimbia kwenu kusiwe katika aharaka, bali mambo yote yatengenezwe mbele yenu; na yule aendaye, na basiangalie nyuma lisije angamizo la ghafla likaja juu yake.

16 Sikilizeni na msikie, Enyi wakazi wa dunia. aSikieni kwa pamoja, ninyi wazee wa kanisa langu, na msikie sauti ya Bwana; kwani awaita watu wote, naye huwaamuru watu wote kila mahali bkutubu.

17 Kwani tazama, Bwana Mungu aamemtuma malaika akilia katikati ya mbingu, akisema: Itengenezeni njia ya Bwana, na byanyoosheni mapito yake, kwani saa ya ckuja kwake imekaribia—

18 Wakati aMwanakondoo atakaposimama juu ya bMlima Sayuni, na pamoja naye watu cmia arobaini na nne elfu, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

19 Kwa hiyo, jitayarisheni kwa ajili ya aujio wa bBwana harusi; nendeni, nendeni nje kumlaki.

20 Kwani tazama, aatasimama juu ya mlima wa Mizeituni, na juu ya bahari kuu, hata vilindi vikuu, na juu ya visiwa vya bahari, na juu ya nchi ya Sayuni.

21 Naye aatatoa sauti yake toka bSayuni, naye atasema kutoka Yerusalemu, na sauti yake itasikika miongoni mwa watu wote;

22 Na itakuwa kama asauti ya maji mengi, na kama sauti ya bradi kuu, ambayo citaivunja milima, na mabonde hayataonekana.

23 Ataviamuru vilindi vikuu, navyo vitasukumwa kurudi katika nchi za kaskazini, na avisiwa vitakuwa nchi moja;

24 Na nchi ya aYerusalemu na nchi ya Sayuni zitarudishwa katika mahali pao, na dunia itakuwa kama ilivyokuwa katika siku zile kabla ya bkugawanyika.

25 Na Bwana, hata Mwokozi, atasimama katikati ya watu wake, naye aatatawala juu ya wote wenye mwili.

26 Nao walioko katika nchi za akaskazini watakumbukwa mbele za Bwana; na manabii wao wataisikia sauti yake, nao hawataweza tena kujizuia; nao wataipiga miamba, na barafu itatiririka mbele ya uwepo wao.

27 Na anjia kuu itainuliwa katikati ya vilindi vikuu.

28 Maadui zao watakuwa mawindo kwao,

29 Na katika jangwa akame yatajitokeza mabwawa ya maji ya uzima; na ardhi kavu haitakuwa tena nchi yenye kiu.

30 Nao wataleta hazina za utajiri wao kwa watoto wa aEfraimu, mtumishi wangu.

31 Na mipaka ya avilima isiyo na mwisho itatetemeka mbele ya uwepo wao.

32 Na hapo wataanguka chini na kuvikwa taji la utukufu, hata katika Sayuni, kwa mikono ya watumishi wa Bwana, hata watoto wa Efraimu.

33 Nao watajawa na anyimbo za shangwe isiyo na mwisho.

34 Tazama, hii ndiyo baraka ya Mungu asiye na mwisho juu ya amakabila ya Israeli, na baraka iliyo kuu juu ya kichwa cha bEfraimu na wenzake.

35 Na wao pia wa kabila la aYuda, baada ya machungu yao watatakaswa katika butakatifu mbele za Bwana, ili kukaa mbele za uwepo wake mchana na usiku, milele na milele.

36 Na sasa, amini hivi ndivyo asema Bwana, ili mambo haya yapate kujulikana miongoni mwenu, Enyi wakazi wa dunia, nimemtuma amalaika wangu akiruka katikati ya mbingu, mwenye binjili isiyo na mwisho, ambaye amewatokea baadhi na kuikabidhi kwa mwanadamu, ambaye ataonekana kwa wengi wale wakaao duniani.

37 Na ainjili hii bitahubiriwa kwa ckila taifa, na kabila, na lugha, na watu.

38 Na watumishi wa Mungu watakwenda, wakisema kwa sauti kubwa: Mcheni Mungu na mtukuzeni yeye, kwa maana saa ya hukumu yake imefika;

39 Na amwabuduni yeye aliyezifanya mbingu, na dunia, na bahari, na chemi chemi za maji—

40 Mkililingana jina la Bwana mchana na usiku, mkisema: Ee laiti aungepasua mbingu, ili ushuke ili milima ipate kutiririka mbele zako.

41 Na itajibiwa juu ya vichwa vyao; kwa maana uwepo wa Bwana utakuwa kama moto wenye kuyeyuka unaowaka uunguzao, na kama moto ufanyao maji akuchemka.

42 Ee Bwana, utashuka chini ili kuwajulisha adui zako jina lako, na mataifa yote yatatetemeke mbele zako—

43 Unapofanya mambo ya kutisha, mambo wasiyoyatazamia;

44 Ndiyo, ushukapo, na milima kutiririka mbele zako, wewe awamlaki yeye afurahiaye yaliyo ya haki na kuyatenda, wale wakukumbukao katika njia zako.

45 Maana tangu mwanzo wa ulimwengu watu hawakusikia wala kufahamu kwa masikio, wala jicho lolote halikuona, Ee Mungu, zaidi yako wewe, ni mambo gani makuu auliyoyaandaa kwa ajili yake yeye bakungojae wewe.

46 Na itasemwa: Ni anani yule bashukaye kutoka kwa Mungu mbinguni mwenye mavazi yaliyotiwa rangi; ndiyo, kutoka sehemu zisizojulikana, aliyevikwa katika mavazi yake matukufu, akitembea katika ukuu wa nguvu zake?

47 Naye atasema: Mimi ndiye niliyenena katika haki, mwenye nguvu ya kuokoa.

48 Naye Bwana atakuwa amwekundu katika mavazi yake, na nguo zake kama za yule akanyagaye katika pipa la mvinyo.

49 Na uwepo wake utakuwa na utukufu mkubwa kiasi kwamba ajua litauficha uso wake kwa aibu, na mwezi itaizuia nuru yake, nazo nyota zitaondoshwa kutoka mahali pake.

50 Na sauti yake itasikika: aNalikanyaga shinikizo la mvinyo pekee yangu, na nimeileta hukumu juu ya watu wote; na hakuna hata mmoja aliyekuwa pamoja nami;

51 Na nimewavyoga katika ghadhabu yangu, na nikawakanyaga katika hasira yangu, na damu yao anikainyunyizia kwenye mavazi yangu, nayo imeharibu vazi langu lote; kwani hii ilikuwa siku ya kulipa kisasi kilichokuwa moyoni mwangu.

52 Na sasa mwaka wa waliokombolewa wangu umefika; nao watataja ukarimu wa Bwana wao, na yote ambayo ameyaweka juu yao kulingana na wema wake, na kulingana na ukarimu wake, milele na milele.

53 Katika amateso yao yote yeye aliteswa. Na malaika wa uwepo wake akawaokoa; na katika bupendo wake, na katika huruma yake, cakawakomboa, na aliwasaidia, na kuwabeba siku zote za kale;

54 Ndiyo, na aHenoko pia, na wale waliokuwa pamoja naye; manabii waliokuwa kabla yake; na bNuhu pia, na wale waliokuwa kabla yake; na cMusa pia, na wale waliokuwa kabla yake;

55 Na tangu Musa hadi Eliya, na tangu Eliya hadi Yohana, waliokuwa pamoja na Kristo katika aufufuko wake, na mitume watakatifu, pamoja na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, watakuwa katika uwepo wa Mwanakondoo.

56 Na amakaburi ya bwatakatifu cyatafunguliwa; nao wataamka na kusimama dmkono wa kuume wa Mwanakondoo, wakati atakaposimama juu ya eMlima Sayuni, na juu ya mji mtakatifu, fYerusalemu Mpya; nao wataimba gwimbo wa hMwanakondoo, mchana na usiku milele na milele.

57 Na kwa sababu hii, ili wanadamu wapate kufanywa washiriki wa autukufu ambao utafunuliwa, Bwana aliupeleka utimilifu wa binjili yake, agano lake lisilo na mwisho, wakisemezana kwa uwazi na urahisi—

58 Kuwaandaa walio dhaifu kwa ajili ya mambo yale yajayo duniani, na kwa ajili ya kazi ya Bwana katika siku ile walio awapumbavu watakapo washinda wenye hekima, na bmnyonge atakapokuwa taifa hodari, na cwawili watawafanya makumi elfu wao kuwakimbia.

59 Na kwa walio wadhaifu wa dunia Bwana aatayapura mataifa kwa uwezo wa Roho wake.

60 Na ni kwa ajili hii amri hizi zilitolewa; ziliamriwa kuzuiliwa kuja ulimwenguni katika siku ile zilipotolewa, lakini sasa aziende kwa bwote wenye mwili—

61 Na hii ni kulingana na nia na mapenzi ya Bwana, atawalaye juu ya wenye mwili wote.

62 Na kwake yeye aatubuye na bkujitakasa mwenyewe mbele za Bwana atapewa cuzima wa milele.

63 Na juu yao wale awasiosikiliza sauti ya Bwana litatimizwa lile lililoandikwa na nabii Musa, kwamba bwatakatiliwa mbali kutoka miongoni mwa watu.

64 Na pia lile lililoandikwa na nabii aMalaki: Kwa maana, tazameni, siku ile binakuja citakayowaka kama tanuri, na wote wenye kiburi, ndiyo, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi, hata haitawaachia mzizi wala tawi.

65 Kwa hiyo, hili ndilo litakuwa jibu la Bwana kwao:

66 Katika siku ile nilipokuja kwa walio wangu, hakuna mtu miongoni mwenu aaliyenipokea, nanyi mlifukuzwa.

67 Nilipoita tena hapakuwa na yeyote kati yenu wa kunijibu; lakini amkono wangu haukuwa mfupi kwa namna yoyote kwamba nisiweze kukomboa, wala buwezo wangu wa kukomboa.

68 Tazama, kwa kemeo langu aninaikausha bahari. Naifanya mito kuwa jangwa; samaki wao kunuka, na kufa kwa kiu.

69 Nazivika mbingu kwa weusi, nafanya nguo ya gunia kuwa mavazi yake.

70 Na ahili mtalipata kutoka mikononi mwangu—mtalala chini kwa huzuni.

71 Tazama, na lo, hakuna wa kuwakomboa ninyi; kwa kuwa hamkutii sauti yangu wakati nilipokuiteni kutoka mbinguni; hamkuwaamini watumishi wangu, na awalipoletwa kwenu hamkuwapokea.

72 Kwa hiyo, waliutia amuhuri ushuhuda na kuifunga sheria, nanyi mkaachwa gizani.

73 Hawa watakwenda katika giza la nje, ambako kuna akilio, na kuomboleza, na kusaga meno.

74 Tazama Bwana Mungu wenu amenena hilo. Amina.