Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 77


Sehemu ya 77

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii huko Hiram, Ohio, kama Machi 1832. Historia ya Joseph Smith inaeleza, “Kuhusiana na tafsiri, ya Maandiko, nilipokea ufafanuzi ufuatao wa Ufunuo wa Mt. Yohana.”

1–4, Wanyama wana roho na wataishi katika furaha ya milele juu ya dunia isiyo kufa; 5–7, Dunia hii itaishi kwa muda wa miaka 7000; 8–10, Malaika mbalimbali huirejesha injili na kuhudumu duniani; 11, Waliotiwa muhuri kwa 144,000; 12–14, Kristo atakuja mwanzoni mwa miaka ya elfu saba; 15, Manabii wawili watainuliwa kwa taifa la Israeli.

1 S. aBahari ya kioo iliyozungumzwa na Yohana, mlango 4 na mstari wa 6 wa Ufunuo ni nini?J. Ni bdunia, katika hali yake ya kutakaswa, isiyokufa, na ya cmilele.

2 S. Tuelewe nini kwa wanyama wanne, waliozungumzwa katika mstari huo huo?J. Ni maneno ya aishara, yaliyotumiwa na Mfunuzi, Yohana, katika kueleza bmbingu, cpeponi ya Mungu, dfuraha ya mwanandamu, na ya wanyama, na ya vitu vitambaavyo, na ya ndege wa angani; na kile kilicho kiumbe cha kiroho katika kufanana na kile kilicho cha kimwili; na kile kiumbe cha kimwili katika kufanana na kile cha kiroho; eroho ya mwanadamu katika kufanana na mwili wake, vivyo hivyo pia roho ya fmnyama, na kila kiumbe ambacho Mungu amekiumba.

3 S. Je, wanyama wale wanne inamaanisha wanawakilisha wanyama maalumu tu, au wanawakilisha wanyama mbalimbali?J. Wanawakilisha wanyama maalumu wanne, ambao walionyeshwa kwa Yohana, ili kuwakilisha utukufu wa makundi ya viumbe katika mpangilio wao uliokusudiwa au aeneo la uumbaji, katika kufurahia bfuraha yao ya milele.

4 S. Tuelewe nini kwa macho na mabawa ambayo wanyama wale walikuwa nayo?J. Macho yao yanawakilisha nuru na amaarifa, maana yake, wamejaa maarifa; na mabawa yao yanawakilisha buwezo, wa kutembea, wa kutenda, na kadhalika.

5 S. Tuelewe nini kwa awazee ishirini na wanne, waliozungumzwa na Yohana?J. Tuelewe kuwa wazee hawa aliowaona Yohana, walikuwa wazee waliokuwa bwaaminifu katika kazi ya huduma na walikufa; na walikuwa wa makanisa yale csaba, na walikuwa katika peponi ya Mungu.

6 S. Tuelewe nini kwa kitabu ambacho Yohana alikiona, ambacho kilikuwa kimetiwa alakiri nyuma kwa lakiri saba?J. Tuelewe kuwa inajumuisha mapenzi yaliyofunuliwa, bsiri, na kazi za Mungu; mambo yake yaliyofichika ya utawala wake kuhusu cdunia katika kipindi cha miaka elfu saba cha kudumu kwake, au katika uhai wake.

7 S. Tuelewe nini kwa lakiri saba zlizotiwa?J. Tuelewe kuwa muhuri wa kwanza ni juu ya mambo ya miaka aelfu moja ya kwanza, na wa pili pia ni juu ya miaka elfu ya pili, na kuendelea hadi wa saba.

8 S. Tuelewe nini kwa malaika wanne, waliozungumzwa katika mlango wa 7 na mstari wa 1 wa Ufunuo?J. Tuelewe kuwa ni malaika wanne waliotumwa kutoka kwa Mungu, ambao wamepewa uwezo juu ya pembe nne za nchi, kuponya uhai au kuangamiza; hawa ndiyo wale wenye ainjili isiyo na mwisho ya kuhubiri kwa kila taifa, kabila, lugha, na watu; wakiwa na uwezo wa kuzifunga mbingu, kuwafungia maisha, au kuwatupa chini bsehemu ya giza.

9 S. Tuelewe nini kwa malaika kushuka kutoka mashariki, Ufunuo mlango wa 7 na mstari wa 2?J. Tuelewe kuwa malaika ashukaye kutoka mashariki ni yule aliyepewa muhuri wa Mungu aliye hai kwa ajili ya makabila kumi na mawili ya aIsraeli; kwa hiyo, akilia kwa malaika wanne wenye injili isiyo na mwisho, akisema: Msidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapo kwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya bvipaji vya nyuso zao. Na, ikiwa mtaipokea, huyu ndiye cElia atakayekuja kuyakusanya pamoja makabila ya Israel na dkurejesha mambo yote.

10 S. Mambo yaliyozungumzwa katika mlango huu yatamalizika wakati gani?J. Yatamalizika katika kipindi cha miaka aelfu sita, au kufunguliwa kwa lakiri ya sita.

11 S. Tuelewe nini kwa kutiwa muhuri kwa watu amia moja na arobaini na nne elfu kutoka makabila yote ya Israeli—kumi na wawili elfu kutoka kila kabila?J. Tuelewe kuwa wale waliotiwa muhuri ni bmakuhani wakuu, waliotawazwa katika mpango mtakatifu wa Mungu! kusimamia injili isiyo na mwisho; kwani wao ndiyo waliotawazwa kutoka kila taifa, kabila, lugha, na watu, na malaika ambao walipewa uwezo juu ya mataifa ya dunia, kuwaleta wengi kadiri iwezekanavyo katika kanisa la cMzaliwa wa Kwanza.

12 S. Tuelewe nini kwa kupigwa kwa amabaragumu, yaliyotajwa katika mlango wa 8 wa Ufunuo?J. Tuelewe kuwa kama vile Mungu alivyoumba ulimwengu katika siku sita, na siku ya saba akamaliza kazi yake, na bakaitakasa, na pia akamtengeneza mwanadamu kutoka cmavumbi ya dunia, hata hivyo, mwanzoni mwa miaka elfu saba Bwana Mungu dataitakasa dunia, na kukamilisha wokovu wa mwanadamu, na ekuvihukumu vitu vyote, na fatavikomboa vitu vyote, isipokuwa kile ambacho hakukiweka ndani ya uwezo wake, wakati atakapokuwa amekwisha tia muhuri vitu vyote, hata mwisho wa vitu vyote; na kupigwa kwa parapanda za malaika saba ni kutayarisha na kumalizika kwa kazi yake, mwanzoni mwa miaka ya elfu saba—kutayarisha njia kabla ya wakati wa kuja kwake.

13 S. Ni lini yatatimizwa mambo yaliyoandikwa katika mlango wa 9 wa Ufunuo?J. Yatatimizwa baada ya kufunguliwa kwa lakiri ya saba, kabla ya kuja kwa Kristo.

14 S. Tuelewe nini kwa kitabu kidogo akilicholiwa na Yohana, kama ilivyotajwa katika mlango wa 10 wa Ufunuo?J. Tuelewe kuwa ilikuwa ni kazi na ibada, kwake yeye ya bkuyakusanya makabila ya Israeli; tazama, huyu ndiye Elia, ambaye, kama ilivyoandikwa, ni lazima atakuja naye catarejesha mambo yote.

15 S. Nini kieleweke kwa amashahidi wawili, katika mlango wa kumi na moja ya Ufunuo?J. Ieleweke kuwa ni manabii wawili ambao watainuliwa kwa btaifa la Kiyahudi katika csiku za mwisho, wakati wa durejesho, na wa kutoa unabii kwa Wayahudi baada ya kukusanywa na kujenga mji wa Yerusalemu katika enchi ya baba zao.