Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 43


Sehemu ya 43

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, Februari 1831. Kwa wakati huu baadhi ya waumini wa Kanisa walikuwa wakisumbuliwa na watu waliokuwa wakijifanya wao kuwa ni wafunuzi. Nabii alimwomba Bwana na kupokea mawasiliano haya yaliyoelekezwa kwa wazee wa Kanisa. Sehemu ya kwanza hushughulika na masuala ya utawala wa Kanisa; sehemu ya mwisho ina maonyo ambayo wazee lazima wayatoe kwa mataifa ya ulimwengu.

1–7, Mafunuo na amri huja tu kupitia mteule mmoja; 8–14, Watakatifu wanatakaswa kwa kutenda katika utakatifu wote mbele za Bwana; 15–22, Wazee wanatumwa kuhubiri toba na kuwatayarisha watu kwa ajili ya siku kuu ya Bwana; 23–28, Bwana huwaita watu kwa sauti Yake mwenyewe na kwa nguvu za asili; 29–35, Milenia na kufungwa kwa Shetani vitakuja.

1 Ee sikilizeni, ninyi wazee wa kanisa langu, na mtege sikio kwa maneno ambayo nitayasema kwenu.

2 Kwani tazama, amini, amini ninawaambia, kwamba mmeipokea amri kama asheria kwa kanisa langu, kupitia yule ambaye nimemteua kwenu kupokea bamri na mafunuo kutoka mikononi mwangu.

3 Kwa hakika jueni—kwamba hakuna mwingine yeyote aliyeteuliwa kwenu kupokea amri na mafunuo hadi atakapochukuliwa, kama aatakaa ndani yangu.

4 Lakini amini, amini, ninawaambia, kwamba ahakuna mwingine yeyote atakayeteuliwa kupokea kipawa hiki isipokuwa iwe kupitia kwake; kwani kama kitachukuliwa kutoka kwake hatakuwa na uwezo isipokuwa kumteua mwingine mahali pake.

5 Na hii itakuwa sheria kwenu, kwamba msipokee mafundisho ya yeyote yatakayokuja mbele yenu kama mafunuo au amri;

6 Na hii ninaitoa kwenu ili msiweze akudanganyika, kwamba muweze kujua kwamba siyo wangu.

7 Kwani amini ninawaambia kwamba yule ambaye aametawazwa na Mimi ataingia bmlangoni na atatawazwa kama nilivyowaambia hapo awali, kufundisha mafunuo yale ambayo mmeyapokea na mtakayopokea kupitia kwake yeye niliyemteua.

8 Na sasa, tazama, ninawapa ninyi amri, kwamba wakati mkikusanyika pamoja amtaelekezana na kuinuana ninyi kwa ninyi, ili muweze kujua namna ya kutenda na kulielekeza kanisa langu, namna ya kutenda juu ya mafundisho ya sheria na amri zangu, ambazo nimewapa.

9 Na hivyo ndivyo mtafundishwa katika sheria ya kanisa langu, na amtakaswe kwa kile mlichokipokea, nanyi mtajifunga wenyewe kutenda katika utakatifu wote mbele zangu—

10 Kwamba kadiri mtakavyofanya haya, utukufu autaongezwa kwenye ufalme ambao mmepokea. Kadiri msivyo yafanya haya, bkitachukuliwa, hata ambacho mmekipokea.

11 Safisheni auovu ulioko miongoni mwenu; jitakaseni wenyewe mbele yangu;

12 Na kama mnataka utukufu wa ufalme, mkubalini mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na amuungeni mkono yeye mbele yangu kwa sala ya imani.

13 Na tena, ninawaambia, kwamba kama mnataka asiri za ufalme, mpatieni chakula na mavazi, na vitu vyote ahitajivyo kukamilisha kazi ambayo nimemwamuru;

14 Na kama hamtayafanya atabakia kwao waliompokea, ili niweze kuhifadhia watu walio asafi mbele zangu.

15 Tena ninasema, sikilizeni ninyi wazee wa kanisa langu, ambao nimewateua: Hamjatumwa akufundishwa, bali kufundisha wanadamu mambo ambayo nimeyaweka mikononi mwenu kwa uwezo wa bRoho wangu;

16 Na amtafundishwa kutoka juu. bJitakaseni na cmtajaliwa uwezo, ili muweze kutoa kama nilivyonena.

17 Sikilizeni ninyi, kwani, tazama, asiku ile bkuu ya Bwana imekaribia.

18 Kwani siku yaja ambayo Bwana atatoa asauti yake toka mbinguni; mbingu bzitatikisika na nchi citatetemeka, na dparapanda ya Mungu italia kwa sauti yenye kuendelea na kwa sauti, na atasema kwa mataifa yaliyolala: ninyi watakatifu eamkeni na muishi; ninyi wenye dhambi fbakini na gmlale hadi nitakapoita tena.

19 Kwa hiyo fungeni viuno vyenu msije kukutwa miongoni mwa waovu.

20 Piga kelele na usiache. Yaiteni mataifa kutubu, wazee kwa vijana, wafungwa na walio huru, mkisema: Jitayarisheni wenyewe kwa siku ile kuu ya Bwana;

21 Kwani kama Mimi, niliye mwanadamu, napiga kelele na kuwaita ninyi kutubu, na mnanichukia, mtasema nini wakati siku ile itakapokuja wakati ngurumo ya aradi itakapotoa ngurumo kutoka miisho ya dunia, ikisema kwenye masikio ya wale wote walio hai, ikisema—Tubuni, na jitayarisheni kwa ajili ya siku ile kuu ya Bwana?

22 Ndiyo, na tena, wakati vimulimuli vya radi vitakapomulika kutoka mashariki hadi magharibi, na kutoa sauti zao kwa wale wote waishio, na kufanya masikio ya wote kuwaka ya wale wenye kusikia, zikisema maneno haya—Tubuni ninyi, kwani siku ile kuu ya Bwana imekuja?

23 Na tena, Bwana atatoa sauti yake kutoka mbinguni, akisema: Sikieni, Enyi mataifa ya dunia, na yasikilizeni maneno ya yule Mungu aliyewaumba ninyi.

24 Ee, ninyi mataifa ya dunia, ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja kama vile akuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini bhamkutaka!

25 Na ni mara ngapi animewaita ninyi kwa vinywa vya bwatumishi wangu, na kwa ckutembelewa na malaika, na kwa sauti yangu mwenyewe, na kwa sauti ya ngurumo za radi, na kwa sauti ya radi, na kwa sauti za tufani, na kwa sauti za matetemeko ya ardhi, na kwa tufani ya mvua ya mawe, na kwa sauti za dnjaa, na madhara ya kila aina, na kwa sauti kuu ya parapanda, na kwa sauti ya hukumu, na kwa sauti ya ehuruma kwa siku nzima, na kwa sauti ya utukufu na heshima na utajiri wa uzima wa milele, na ningewaokoa kwa wokovu fusio na mwisho, lakini hamkutaka!

26 Tazama, siku imekuja, wakati kikombe cha ghadhabu ya uchungu wa hasira yangu kimejaa.

27 Tazama, amini ninawaambia, kwamba haya ni maneno ya Bwana Mungu wenu.

28 Kwa hivyo, fanyeni kazi, afanyeni kazi katika shamba langu la mizabibu kwa mara ya mwisho—kwa mara ya mwisho waiteni wakazi wa dunia hii.

29 Kwani katika saa yangu mwenyewe anitakuja juu ya dunia katika hukumu, na watu wangu watakombolewa na watatawala pamoja nami duniani.

30 Kwani ile aMilenia kuu, ambayo niliinena kwa vinywa vya watumishi wangu itakuja.

31 Kwani aShetani atakuwa bamefungwa, na wakati atakapoachiliwa tena atatawala kwa ckipindi kifupi tu, na hapo ndipo dmwisho wa dunia utakapokuja.

32 Na yule ambaye anaishi katika ahaki batabadilishwa katika kufumba na kufumbua macho, na dunia itapita kama vile kwa moto.

33 Na waovu watakwenda zao katika amoto usiozimika, na mwisho wao hakuna mtu aujuaye hapa duniani, wala kamwe hatajua, hadi watakapokuja mbele yangu katika bhukumu.

34 Sikilizeni ninyi maneno haya. Tazama, Mimi ni Yesu Kristo, aMwokozi wa ulimwengu. bYatunzeni mambo haya katika mioyo yenu, na ctaadhima ya milele diwe eakilini mwenu.

35 Kuweni amakini. Shikeni amri zangu zote. Hivyo ndivyo. Amina.