Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 61


Sehemu ya 61

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, kwenye kingo ya Mto Missouri, sehemu ya McIlwaine’s Bend, 12 Agosti 1831. Katika safari yao ya kurejea Kirtland, Nabii na wazee kumi walisafiri kwa mitumbwi katika Mto Missouri. Mnamo siku ya tatu ya safari yao, waliona hatari nyingi. Mzee William W. Phelps, katika ono la mchana, aliona mharibifu akitembea kwa nguvu juu ya uso wa maji.

1–12, Bwana ametangaza uangamiaji mkubwa juu ya maji; 13–22, Maji yalilaaniwa na Yohana, na mharibifu hutembea juu ya uso wake; 23–29, Wengine wana uwezo wa kuyaamuru maji; 30–35, Wazee wasafiri wawili wawili na kuhubiri injili; 36–39, Wanapaswa kujiandaa kwa ajili ya kuja kwake Mwana wa Mtu.

1 Tazama, na sikilizeni sauti yake yeye aliye na auwezo wote, aliye tangu milele hata milele, bAlfa na Omega, mwanzo na mwisho.

2 Tazama, amini hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwenu, Enyi wazee wa kanisa langu, mliokusanyika mahali hapa, ninyi ambao dhambi zenu zimesamehewa sasa, kwani Mimi, Bwana, ahusamehe dhambi, na ni mwenye bhuruma kwa wale ambao chuziungama dhambi zao kwa moyo mnyenyekevu;

3 Lakini amini ninawaambia, kwamba haifai kwa kundi lote hili la wazee kusafiri kwa haraka juu ya maji, wakati wakazi wa pande zote mbili wanaangamia katika kutoamini.

4 Hata hivyo, niliruhusu ili kwamba muweze kushuhudia; tazama, kuna hatari nyingi juu ya maji, na hasa hapo baadaye;

5 Kwani Mimi, Bwana, nimetangaza katika hasira yangu maangamizi mengi juu ya maji; ndiyo, na hususani juu ya maji haya.

6 Hata hivyo, wenye mwili wako katika mikono yangu, na yule aliye mwaminifu miongoni mwenu hataangamia kwa maji.

7 Kwa hivyo, yafaa kuwa mtumishi wangu Sidney Gilbert na mtumishi wangu aWilliam W. Phelps wafanye haraka kwenda kwenye kazi yao na huduma yao.

8 Hata hivyo, nisingeliwaacha mtawanyike hadi muwe animewaadhibu kwa ajili ya dhambi zenu zote, ili mpate kuwa na umoja, ili msiweze kuangamia katika buovu;

9 Lakini sasa, amini ninawaambia, ni muhimu kwangu kwamba yawapasa kutawanyika. Kwa hivyo watumishi wangu Sidney Gilbert na William W. Phelps waende na kundi lao la awali, na wafanye safari yao kwa haraka ili waweze kutimiza huduma yao, na kwa kupitia imani yao watashinda;

10 Na kwa kadiri watakavyokuwa waaminifu watalindwa, na Mimi, Bwana, nitakuwa pamoja nao.

11 Na waliosalia wachukue mavazi wanayohitaji.

12 Na mtumishi wangu Sidney Gilbert achukue yale yasiyohitajika pamoja naye, kama mtakavyokubaliana.

13 Na sasa, tazama, kwa afaida yenu nilitoa bamri kwenu juu ya mambo haya; na Mimi, Bwana, nitasemezana nanyi kama vile watu wa siku za kale.

14 Tazama, Mimi, Bwana, mwanzoni niliyabariki amaji; lakini katika siku za mwisho, kwa kinywa cha mtumishi wangu Yohana, bniliyalaani maji.

15 Kwa hiyo, siku zitakuja ambapo hakuna kiumbe kitakachokuwa salama juu ya maji.

16 Na itasemwa katika siku zijazo kwamba hakuna awezaye kwenda katika nchi ya Sayuni juu ya maji, ila yule aliye safi moyoni.

17 Na, kama vile Mimi, Bwana, mwanzoni aniliilaani ardhi, hata hivyo katika siku za mwisho nimeibariki, katika wakati wake, kwa ajili ya matumizi ya watakatifu wangu, ili waweze kushiriki unono wake.

18 Na sasa ninatoa kwenu amri kwamba lile nilisemalo kwa mmoja ninalisema kwa wote, kwamba mtawaonya ndugu zenu kuhusu maji haya, ili wasije wakasafiri katika maji haya, na imani yao itindike, nao wakanaswa katika mitego;

19 Mimi, Bwana, nimelitangaza na mwangamizaji anatembea juu ya uso wake, na Mimi sifuti tangazo hilo.

20 Mimi, Bwana, niliwakasirikia jana, lakini leo hasira yangu imegeuka.

21 Kwa hiyo, na wale ambao nimezungumza juu yao, kuwa wafunge safari zao upesi—na tena ninawaambia, wafunge safari zao upesi.

22 Na hii sijali, hata kama itakuwa baada ya kitambo kidogo, ili mradi wametimiza wajibu wao, iwe wamekwenda kwa njia ya maji au nchi kavu; na iwe kama inavyofahamika kwao kulingana na maamuzi yao hapo baadaye.

23 Na sasa, kuhusu watumishi wangu, Sidney Rigdon, Joseph Smith, Mdogo, na Oliver Cowdery, wasije tena juu ya maji, isipokuwa iwe juu ya mfereji, wakati wakisafiri kwenda majumbani kwao; au katika maneno mengine hawatakuja juu ya maji kwa ajili ya kusafiri, isipokuwa juu ya mfereji.

24 Tazama, Mimi, Bwana, nimeonyesha njia kwa ajili ya kusafiri kwa watakatifu wangu; na tazama, hii ndiyo njia—kwamba baada ya kuondoka kwenye mfereji watasafiri kwa nchi, kadiri ya vile watakavyoamuriwa kusafiri na kuelekea kwenye nchi ya Sayuni;

25 Nao watafanya kama wana wa Israeli, awakipiga mahema yao wakiwa njiani;

26 Na, tazama, amri hii mtaitoa kwa ndugu zenu wote.

27 Hata hivyo, kwa yule ambaye auwezo umetolewa kwake kuyaamuru maji, kwake imetolewa kwa njia ya Roho kuzijua njia zake zote;

28 Kwa hiyo, na afanye vile Roho wa Mungu aliye hai anavyomwamuru, iwe juu ya nchi kavu au juu ya maji, kama ilivyobakia kwangu kufanya hapo baadaye.

29 Na kwenu ninyi imetolewa njia kwa ajili ya watakatifu, au njia kwa ajili ya watakatifu wa jeshi la Bwana, kusafiri.

30 Na tena, amini ninawaambia, watumishi wangu Sidney Rigdon, Joseph Smith, Mdogo, na Oliver Cowdery, hawatafungua vinywa vyao katika makusanyiko ya waovu hadi watakapofika huko Cincinnati;

31 Na katika mahali hapo watapaza sauti zao kwa Mungu dhidi ya watu wale, ndiyo, kwake yeye ambaye hasira yake inawaka dhidi ya uovu wao, watu ambao karibu awameiva kwa angamizo.

32 Na kutoka hapo wasafiri kwenda kwenye mkutano wa ndugu zao, kwani kazi zao hata sasa zatakiwa sana miongoni mwao kuliko miongoni mwa makusanyiko ya waovu.

33 Na sasa, kuhusu waliosalia, nao wasafiri na akulitangaza neno miongoni mwa mikutano ya waovu, kadiri vile itakavyotolewa;

34 Na kadiri watakavyofanya hivi watakuwa awakiyaosha mavazi yao, nao watakuwa hawana waa mbele zangu.

35 Nao wasafiri pamoja, au awawili wawili, kama waonavyo wao kuwa ni vyema, isipokuwa tu mtumishi wangu Reynolds Cahoon, na mtumishi wangu Samuel H. Smith, ambao ninapendezwa nao, wasitenganishwe hadi watakaporudi majumbani kwao, na hii ni kwa sababu ya hekima iliyo kwangu.

36 Na sasa, amini ninawaambia, na lile nisemalo kwa mmoja nasema kwa wote, muwe na furaha, awatoto wadogo; kwani mimi nipo bkatikati yenu, na csijawasahau;

37 Na kadiri mnavyojinyenyekeza wenyewe mbele zangu, baraka za aufalme ni zenu.

38 Vifungeni viuno vyenu na muwe awaangalifu na kuwa na kiasi, mkitazamia kuja kwa Mwana wa Mtu, kwani yuaja katika saa msiodhania.

39 aOmbeni daima ili msije mkaingia bmajaribuni, ili muweze kustahimili siku ya kuja kwake, iwe katika uzima au katika mauti. Hivyo ndivyo. Amina.