Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 34


Sehemu ya 34

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Orson Pratt, huko Fayette, New York, 4 Novemba 1830. Ndugu Pratt alikuwa na umri wa miaka kumi na tisa wakati huo. Alikuwa ameongoka na kubatizwa wakati aliposikia kuhubiriwa kwa injili iliyorejeshwa kwa mara ya kwanza iliyohubiriwa na kaka yake mkubwa, Parley P. Pratt, wiki sita kabla. Ufunuo huu ulipokewa katika nyumba ya Peter Whitmer Mkubwa.

1–4, Waaminifu huwa wana wa Mungu kwa njia ya Upatanisho; 5–9, Kuhubiriwa kwa injili hutengeneza njia kwa Ujio wa Pili; 10–12, Unabii huja kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

1 Mwanangu aOrson, sikiliza na usikie na tazama kile Mimi, Bwana Mungu, nitakachokuambia, hata Yesu Kristo Mkombozi wako;

2 Niliye anuru na uzima wa ulimwengu, nuru ingʼaayo gizani wala giza haiitambui;

3 Yeye ambaye aaliupenda ulimwengu hata byeye cakautoa uhai wake mwenyewe, kwamba wale wote watakaoamini waweze kuwa dwana wa Mungu. Kwa sababu hiyo wewe u mwanangu;

4 Na aheri wewe kwa sababu umeamini;

5 Na zaidi umebarikiwa kwa sababu aumeitwa na mimi kuihubiri injili yangu—

6 Kwa kupaza sauti yako kama vile kwa sauti ya parapanda yenye kuendelea na kwa sauti, na atangaza toba kwa kizazi hiki chenye hila na ukaidi, ukiitayarisha njia ya Bwana kwa ajili ya bujio wa pili.

7 Kwani tazama, amini, amini, ninakuambia, asaa i karibu ambayo nitakuja katika bwingu kwa uwezo na utukufu mkuu.

8 Nayo itakuwa asiku kubwa wakati wa kuja kwangu, kwani mataifa yote byatatetemeka.

9 Lakini kabla ya kuja kwa siku ile kuu, jua litatiwa giza, na mwezi utageuka damu; na nyota hazitatoa nuru yake, na nyingine zitaanguka, na uharibifu mkubwa wawangojea waovu.

10 Kwa hiyo inua sauti yako na wala ausiache, kwani Bwana Mungu amesema hayo; hivyo basi toa unabii, na itatolewa kwa buwezo wa Roho Mtakatifu.

11 Na kama wewe ni mwaminifu, tazama, Mimi ni pamoja nawe hadi nitakapokuja—

12 Na amini, amini, ninakuambia, naja upesi, Mimi ndimi Bwana wako na Mkombozi wako. Hivyo ndivyo. Amina.