Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 113


Sehemu ya 113

Majibu ya maswali kadha wa kadha juu ya maandiko ya Isaya, yaliyotolewa na Joseph Smith Nabii, huko au jirani na Far West, Missouri, Machi 1838.

1–6, Shina la Yese, chipukizi litokalo ndani yake, na mzizi wa Yese vinaelezewa; 7–10, Mabaki ya watu wa Sayuni waliotawanywa wanayo haki ya ukuhani nao wanaitwa kurejea kwa Bwana.

1 Shina la aYese anayesemwa katika mstari wa 1, 2, 3, 4 na 5 wa mlango wa 11 wa Isaya ni nani?

2 Amini hivyo ndivyo asemavyo Bwana: Ni Kristo.

3 Chipukizi linalosemwa katika mstari wa kwanza wa mlango wa 11 wa Isaya, ambalo litatoka kwenye Shina la Yese ni nini?

4 Tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana: Ni mtumishi katika mikono ya Kristo, ambaye ni wa sehemu ya uzao wa Yese na vile vile ni wa aEfraimu, au wa nyumba ya Yusufu, ambaye juu yake umewekwa buwezo mwingi.

5 Mzizi wa Yese unaosemwa katika mstari wa 10 wa mlango wa 11 ni nini?

6 Tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana, ni mzaliwa wa ukoo wa Yese, vile vile wa Yusuf, ambaye anayo haki ya ukuhani, na afunguo za ufalme, kuwa kama bbendera, na kwa ajili ya ckukusanyika kwa watu wangu katika siku za mwisho.

7 Maswali yaliyoulizwa na Elias Higbee: Kuna maana gani katika amri iliyoko katika Isaya, mlango wa 52, mstari wa 1, ambayo inasema: Jivike nguvu zako, Ee Sayuni—ni watu gani ambao Isaya aliwataja?

8 Alikuwa akiwaelezea watu wale ambao Mungu atawaita katika siku za mwisho, ambao watashikilia uwezo wa ukuhani kuirejesha tena aSayuni, na wa ukombozi wa Israeli; na kujivika bnguvu zake ni kujivika mamlaka ya ukuhani, ambayo yeye, Sayuni, anayo chaki ya kuzaliwa; pia kurejea kwenye ule uwezo ambao aliupoteza.

9 Tuelewe nini kwa Sayuni kujifungulia vifungo vya shingo yake; mstari wa 2?

10 Tuelewe kwamba mabaki awaliotawanyika wanahimizwa bkumrudia Bwana kutoka kule walikoanguka; na wakifanya hivyo, ahadi ya Bwana ni kwamba atanena nao, au atawapa ufunuo. Ona mistari ya 6, 7, na 8. Vifungo vya shingo yake ni laana ya Mungu juu yake, au mabaki ya Israeli katika hali yao ya kutawanywa miongoni mwa Wayunani.