Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 100


Sehemu ya 100

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii na Sidney Rigdon, huko Perrysburg, New York, tarehe 12 Oktoba 1833. Ndugu hawa wawili, wakiwa mbali na familia zao kwa siku kadhaa, walipatwa na wasi wasi juu yao.

1–4, Joseph na Sidney watahubiri injili kwa ajili ya wokovu wa wanadamu; 5–8, Watapewa saa ile watakayosema; 9–12, Sidney atakuwa msemaji na Joseph atakuwa mfunuzi na mwenye nguvu katika ushuhuda; 13–17, Bwana atawainua watu safi, na watiifu wataokolewa.

1 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwenu, marafiki zangu aSidney na bJoseph, familia zenu ni njema; wako mikononi mwangu, na nitawafanyia nionavyo kuwa ni vyema; kwani ndani yangu kuna uwezo wote.

2 Kwa hiyo, nifuateni, na sikilizeni ushauri nitakaowapa.

3 Tazama, na lo, ninao watu wengi katika eneo hili, katika maeneo ya jirani; na mlango wenye kuleta matokeo yanayotakiwa wakufaa utafunguliwa katika maeneo ya jirani katika nchi za mashariki.

4 Kwa hiyo, Mimi, Bwana, nimewaruhusu ninyi kuja mahali hapa; hivyo niliona ni muhimu kwa awokovu wa wanadamu.

5 Kwa hiyo, amini ninawaambia, pazeni sauti zenu kwa watu hawa; ayasemeni mawazo nitakayoyaweka mioyoni mwenu, na ninyi hamtashindwa mbele za watu;

6 Kwani amtapewa katika saa ile ile, ndiyo, katika wakati ule ule, kile mtakachosema.

7 Lakini amri ninaitoa kwenu, kwamba mtakitangaza kitu chochote amtakachotangaza kwa jina langu, kwa taadhima moyoni, kwa roho ya bunyenyekevu, katika mambo yote.

8 Na ninatoa ahadi hii kwenu, ya kuwa ilimradi mtayatenda haya aRoho Mtakatifu atamwagwa katika kutoa ushuhuda kwa mambo yote mtakayosema ninyi.

9 Na ni muhimu kwangu kwamba wewe, mtumishi wangu Sidney, uwe amsemaji kwa watu hawa; ndiyo, amini, nitakutawaza kwa wito huu, hata kuwa msemaji kwa mtumishi wangu Joseph.

10 Nami nitampa yeye uwezo wa kuwa mwenye nguvu katika aushuhuda.

11 Na nitakupa wewe uwezo wa kuwa mwenye anguvu katika kuyaelezea maandiko yote, ili wewe uwe msemaji kwake, naye atakuwa bmfunuzi kwako, ili uweze kujua uhakika wa mambo yote yahusuyo mambo ya ufalme hapa duniani.

12 Kwa hiyo, endeleeni na safari yenu na mioyo yenu ifurahi; kwani tazameni, na lo, Mimi nipo pamoja nanyi hadi mwisho.

13 Na sasa ninawapa neno juu ya aSayuni. Sayuni bitakombolewa, ingawa yeye anatiwa adabu kwa kipindi kifupi.

14 Ndugu zenu, watumishi wangu aOrson Hyde na John Gould, wako mikononi mwangu; na ilimradi wao wanazishika amri zangu wataokolewa.

15 Kwa hiyo, mioyo yenu na ifarijike; kwani mambo ayote yatafanya kazi kwa pamoja kwa manufaa yao wale watembeao wima, na kwa utakaso wa kanisa

16 Kwani nitajiinulia watu asafi, ambao watanitumikia katika haki.

17 Na wale wote awalilingao jina la Bwana, na kuzishika amri zake, wataokolewa. Hivyo ndivyo. Amina.