Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 9


Sehemu ya 9

Ufunuo uliotolewa kupitia kwa Joseph Smith Nabii kwa Oliver Cowdery, huko Harmony, Pennsylvania, Aprili 1829. Oliver anaonywa kuwa awe mvumilivu na anahimizwa kuridhika na kazi ya uandishi, kwa wakati huu, kama inavyosemwa na mfasiri, kuliko kujaribu kutafsiri.

1–6, Kumbukumbu nyingine za kale bado hazijatafsiriwa; 7–14, Kitabu cha Mormoni kinatafsiriwa kwa kuchunguza na kwa uthibitisho wa kiroho.

1 Tazama, ninakuambia wewe, mwana wangu, kwamba kwa sababu ahukutafsiri kama ulivyotaka kutoka kwangu, na hivyo umeanza bkuandika tena kwa ajili ya mtumishi wangu, Joseph Smith, Mdogo, hivyo ndivyo nipendavyo kwamba uendelee kuandika hadi utakapomaliza kumbukumbu hii, ambayo nimemkabidhi yeye.

2 Na halafu, tazama, akumbukumbu bnyingine ninazo, ambazo nitakupa wewe uwezo ili uweze kusaidia kuzitafsiri.

3 Uwe mvumilivu, mwana wangu, kwani hiyo ni hekima kwangu, na haifai wewe kutafsiri kwa wakati huu.

4 Tazama, kazi ambayo umeitwa kuifanya ni kuandika kwa ajili ya mtumishi wangu Joseph.

5 Na, tazama, nimekunyangʼanya heshima hiyo, kwa sababu hukuendelea kuifanya kama vile ulivyoianza kutafsiri.

6 aUsinungʼunike, mwanangu, kwani hiyo ni hekima kwangu kukutendea namna hiyo.

7 Tazama, wewe hujaelewa; ulidhani ya kuwa Mimi nitakupatia tu wewe, wakati wewe hukutafakari isipokuwa kuniomba Mimi tu.

8 Lakini, tazama, ninakuambia, kwamba unalazimika akulichunguza katika akili yako; ndipo buniulize kama ni sahihi, na kama ni sahihi nitaufanya cmoyo wako duwake ndani yako; kwa njia hiyo, eutahisi kuwa hiyo ni sahihi.

9 Lakini kama siyo sahihi hutapata hisia za namna hiyo, bali amzubao wa mawazo ambayo yatakufanya usahau kitu kile kisicho sahihi; kwa sababu hiyo, huwezi kuandika kile kilicho kitakatifu ila kimetolewa kwako kutoka kwangu.

10 Sasa, kama ungelijua hivi ungeliweza akutafsiri; hata hivyo, haifai kuwa wewe utafsiri sasa.

11 Tazama, ilifaa wakati ulipoanza; lakini aukaogopa, na muda umekwisha pita, na haifai tena sasa;

12 Kwani, huoni kwamba nimempa mtumishi wangu aJoseph nguvu za kutosha, ambazo kwa hizo zatosheleza? Na wala hakuna kati yenu niliye mhukumu.

13 Fanya jambo hili ambalo nimekuamuru, na wewe utastawi. Uwe mwaminifu, na usijiingize katika amajaribu.

14 Simama imara katika akazi ambayo bnimekuitia, na wala unywele wa kichwa chako hautapotea, na wewe cutainuliwa juu siku ya mwisho. Amina.