Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 12


Sehemu ya 12

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Joseph Knight Mkubwa, huko Harmony, Pennsylvania, Mei 1829. Joseph Knight aliamini matamko ya Joseph Smith kuhusiana na kuwa nayo mabamba ya Kitabu cha Mormoni na kazi ya kutafsiri ikiwa inaendelea na mara kadhaa amewahi kutoa msaada wa mali kwa Joseph Smith na mwandishi wake, ambao uliwawezesha wao kuendelea kutafsiri. Kwa maombi ya Joseph Knight, Nabii alimwuliza Bwana na kupata ufunuo huu.

1–6, Wafanya kazi katika shamba la mizabibu watapata wokovu; 7–9, Wale wote wanaotamani na wenye kustahili wanaweza kusaidia katika kazi ya Bwana.

1 Kazi akubwa na ya ajabu i karibu kuja miongoni mwa wanadamu.

2 Tazama, Mimi ndimi Mungu; tiini neno langu, lililo hai na lenye nguvu, kali kuliko upanga wenye makali pande mbili, kwa kugawanya viungo na mafuta yaliyo ndani ya mifupa; kwa hiyo litiini neno langu.

3 Tazama, shamba ni jeupe tayari kwa mavuno; kwa hiyo, yeyote atakaye kuvuna na aingize ndani mundu yake kwa nguvu zake, na kuvuna wakati siku ingali, ili aweze kujiwekea hazina ya wokovu usio na mwisho kwa ajili ya nafsi yake katika ufalme wa Mungu.

4 Ndiyo, yeyote atakayeingiza mundu wake na kuvuna, yeye huyo ameitwa na Mungu.

5 Kwa hiyo, kama utaniomba mimi utapata; kama utabisha utafunguliwa.

6 Sasa, kama ulivyoomba, tazama, ninakuambia, shika amri zangu, na tafuta kuanzisha na kustawisha kusudi la Sayuni.

7 Tazama, ninasema nawe, na pia kwa wale wote walio na hamu ya kuanzisha na kuendeleza kazi hii;

8 Na hakuna yeyote awezaye kusaidia katika kazi hii isipokuwa yule aliye amnyenyekevu na aliyejaa bupendo, akiwa na cimani, dmatumaini na ehisani, akiwa na kiasi katika mambo yote, yatakayoaminiwa katika utunzaji wake.

9 Tazama, Mimi ndimi nuru na uzima wa ulimwengu, nisemaye maneno haya, kwa hiyo sikiliza kwa nguvu zako, na kisha wewe umeitwa. Amina.