Misaada ya Kujifunza
25. Mto Yordani


25. Mto Yordani

Picha
picha 25

Mto Yordani huanzia kaskazini mwa Bahari ya Galilaya, hutiririka ndani yake, na halafu huendelea kusini mwa Bahari ya Chumvi. Picha hii ilipigwa karibu na mdomo wa mto kutoka Bahari ya Galilaya.

Matukio Muhimu: Lutu alijichagulia nyanda za Yordani (Mwa. 13:10–11). Yoshua aliyagawanya maji yake, akiwaruhusu Waisraeli kuvuka kuingia katika nchi ya ahadi (Yos. 3:13–17; 4:1–9, 20–24). Eliya na Elisha waliyagawanya maji yake (2 Fal. 2:5–8, 12–14). Naamani aliponyeshwa ukoma (2 Fal. 5:1–15). Yohana Mbatizaji alibatiza watu wengi, ikiwa ni pamoja na Mwokozi (Mt. 3:1–6, 13–16). (Ona MWM Mto Yordani.)