Misaada ya Kujifunza
1. Mto Nile na Misri


1. Mto Nile na Misri

Picha
picha 1

Uoto wa asili unaoota kando ya kingo za Mto Nile. Katika mahali kama hapa, mama yake Musa alimficha mtoto wake mchanga wa kiume. Ngʼambo yake ni jangwa ambalo limeenea sehemu kubwa ya Misri.

Matukio Muhimu: Nchi hii iligunduliwa na Egipto (Ibr. 1:23–25). Ibrahimu alikwenda Misri (Mwa. 12:10–20; Ibr. 2:21–25). Yusufu aliuzwa katika Misri, akawa mtawala, na akaiokoa familia yake kutokana na njaa (Mwa. 37; 39–46). Wazao wa Yakobo waliishi katika Misri (Mwa. 47; Ku. 1; 12:40). Binti wa Farao alimwokota mtoto Musa katika mto na akamlea (Ku. 2:1–10). Musa aliwaongoza Waisraeli kutoka Misri (Ku. 3–14). Maria, Yusufu na Yesu walienda Misri kwa muda ili kumkimbia Herode (Mt. 2:13–15, 19–21). Katika siku za mwisho, Wamisri watamjua Bwana, naye Bwana ataibariki Misri (Isa. 19:20–25). (Ona MWM Misri.)