Misaada ya Kujifunza
11. Mlima wa Mizeituni


11. Mlima wa Mizeituni

Picha
picha 11

Mandhari hii huangalia mashariki kwenye Mlima wa Mizeituni. Jengo lililoko mbele linaonyesha uwezekano wa kuwa eneo la kiwanja cha Bustani ya Gethsemani. Tarehe 24 Oktoba 1841, Mzee Orson Hyde wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alipanda Mlima wa Mizeituni na kutoa sala ya kinabii ya kuwekwa wakfu kwa ajili ya kurudi kwa watoto wa Ibrahimu na ujenzi wa hekalu.

Matukio Muhimu: Rumi iliiangamiza Yerusalemu katika mwaka 70 B.K. kama ilivyotolewa unabii na Mwokozi kutoka katika Mlima wa Mizeituni (ona JS—M 1:23). Mwokozi atasimama juu ya Mlima wa Mizeituni kabla ya kujitokeza Kwake kwa ulimwengu wote (Ona Zek. 14:3–5; M&M 45:48–53; 133:19–20; MWM Mizeituni, Mlima wa.)