Misaada ya Kujifunza
15. Yeriko


15. Yeriko

Picha
picha 15

Picha hii inaonyesha uoto katika Yeriko ya siku ya leo. Hapo Kale ulikuwa mji uliozungukwa na ukuta katika bonde la Mto Yordani, mita 252 chini ya usawa wa bahari. Ni eneo lenye rutuba kwa kilimo ambapo visitu vya mitende na miti jamii ya michungwa hustawi. Nyuma yake ni Mlima wa kimapokeo wa Majaribu (Mt. 4:1–11).

Matukio Muhimu: Karibu na mahali hapa Yoshua na wana wa Israeli walivuka kwanza Mto Yordani ili kuingia nchi ya ahadi (Yos. 2:1–3; 3:14–16). Bwana kimiujiza alisababisha kuta kudondoka mbele ya majeshi ya Israeli (Yos. 6; ona pia Ebr. 11:30). Yoshua aliulaani mji (Yos. 6:26), ambayo ilitimia (1 Fal. 16:34). Elisha aliyaponya maji ya Yeriko (2 Fal. 2:18–22). Mwokozi alipita hapa katika ziara Yakeya mwisho Yerusalemu, akimponya kipofu Bartimayo na kukaa na Zakayo, mtoza ushuru (Mk. 10:46–52; Lk. 18:35–43; 19:1–10). Barabara kwenda Yeriko kutoka Yerusalemu ilitajwa katika mfano wa Msamaria mwena (Lk. 10:30–37). (Ona MWM Yeriko.)