Misaada ya Kujifunza
20. Yafa


20. Yafa

Picha
picha 20

Ukiangalia upande wa Kaskazini magharibi juu ya mji wa bandari wa Yafa.

Matukio Muhimu: Yona alienda Yafa kupanda meli kwenda Tarshishi (Yon. 1:1–3). Yafa ilikuwa ni bandari ambayo Sulemani na baadaye Zerubabeli waliitumia wakati wa kuleta mbao kutoka misitu ya mikangazi ya Lebanoni kwa ajili ya kujenga mahekalu yao (2 Nya. 2:16; Ezra 3:7). Hapa Petro alimfufua Thabita, ambaye anajulikana kama Dorkasi (Mdo. 9:36–43). Petro pia alipata ono la wanyama wasio najisi na walio najisi, akifunuliwa umuhimu wa yeye kuanza huduma miongoni mwa Wayunani (Mdo. 10). Orson Hyde aliwasili hapa ili kuiweka wakfu Nchi Takatifu katika mwaka 1841.