Misaada ya Kujifunza
16. Shilo


16. Shilo

Picha
picha 16

Katika mandhari hii ya magharibi, magofu ya jiji la kale la Shilo kushoto kidogo kutoka katikati ya picha.

Matukio Muhimu: Makabila ya Israeli yalikusanyika hapa na kupokea mgao wao wa eneo la ardhi (Yos. 18–22). Hema na sanduku la agano uliwekwa hapa na ukabaki kwa karne nyingi (Yos. 18:1). Hapa Hana alisali na kumtoa wakfu mwanawe Samweli ili amtumikie Bwana (1 Sam. 1). Waisraeli walilichukua sanduku la agano kutoka Shilo na walishindwa dhidi ya Wafilisti, ambao halafu wakaliteka sanduku la agano (1 Sam. 4:1–11).