Misaada ya Kujifunza
23. Bahari ya Galilaya na Mlima wa Mahubiri ya Heri


23. Bahari ya Galilaya na Mlima wa Mahubiri ya Heri

Picha
picha 23

Ukiangalia Kusini Magharibi kuelekea kona ya Kaskazini magharibi ya Bahari ya Galilaya, ziwa la maji baridi. Kilima cha katikati ya picha ni eneo la kimapokeo la Mlima wa Mahubiri ya Heri. Kapernaumu iko kushoto, nje ya picha. Tiberia iko kushoto zaidi kando kando ya pwani ya magharibi.

Matukio Muhimu: Mwokozi alitumia sehemu kubwa ya huduma Yakekatika mwili wenye kufa katika eneo hili. Hapa aliwaitana kuwatawaza Mitume Kumi na Wawili (Mt. 4:18–22; 10:1–4; Mk. 1:16–20; 2:13–14; 3:7, 13–19; Lk. 5:1–11), alifundisha Mahubiri ya Mlimani (Mt. 5–7), na alifundisha katika mifano (Mt. 13:1–52; Mk. 4:1–34). Miujiza aliyofanyani pamoja na ifuatayo: alimponya wenye ukoma (Mt. 8:1–4); alituliza dhoruba; (Mt. 8:23–27); alifukuza kutoka kwa kijana wa kiume kundi la mapepo, ambao halafu wakawaingia nguruwe ambao walikimbilia baharini (Mk. 5:1–15); aliwalisha watu 5,000 na 4,000 (Mt. 14:14–21; 15:32–38); aliwaamuru wanafunzi wake kutupa nyavu zao, ambapo kwa kufanya hivyo walikamata samaki wengi (Lk. 5:1–6); aliwaponya watu wengi (Mt. 15:29–31; Mk. 3:7–12); alionekana baada ya ufufuko wake ili kuwafundisha wanafunzi wake (Mk. 14:27–28; 16:7; Yn. 21:1–23). (Ona MWM Galilaya.)