Misaada ya Kujifunza
31. Efeso


31. Efeso

Picha
picha 31

Magofu ya jumba la maonyesho ya tamthilia la Uyunani huko Efeso ni mahali ambapo Mtume Paulo alihubiri. Katika nyakati za Agano Jipya, Efeso ulikuwa maarufu katika ulimwengu wote uliojulikana kwa ukubwa wa hekalu lake lililojengwa kwa heshima ya mungu mwanamke wa kipagani wa Kirumi Diana. Sasa ukiwa magofu, Efeso wakati mmoja ulikuwa mji mkuu wa jimbo la Kirumi la Asia na Kituo Kikuu cha biashara. Wafua fedha wa mji waliendeleza biashara ya kuuza sura za Diana.

Matukio Muhimu: Mtume Paulo aliitembelea Efeso karibu ya mwisho wa safari yake ya pili ya Kimisionari (Mdo. 18:18–19). Katika safari yake ya tatu alikaa katika mji huu kwa miaka miwili. Alilazimika kuondoka kwa sababu ya ghasia zilizosababishwa na wafua fedha ambao walikuwa wakipoteza biashara kutokana na Paulo kuhubiri dhidi ya kuabudu mungu mwanamke wa uongo Diana (Mdo. 19:1, 10, 23–41; 20:1). Jumba la maonyesho ya tamthilia la Efeso lilikuwa kubwa zaidi kuliko yote yaliyojengwa na Wayunani na ndipo mahali ambapo mwenza wa Paulo alikabiliana na kundi la wahuni (Mdo. 19:29–31). Paulo aliandika waraka kwa waumini wa Kanisa huko Efeso wakati akiwa amefungwa katika Roma. Moja ya matawi saba ya Kanisa katika Asia ambayo Kitabu cha Ufunuo kimeyataja liko katika Efeso (Ufu. 1:10–11; 2:1).