Misaada ya Kujifunza
28. Dani


28. Dani

Picha
picha 28

Jiji hili la kale la Dani lilikuwa likiitwa Leshemu (Yos. 19:47) au Laishi (Amu. 18:7, 14) kabla ya Waisraeli kuiteka nchi. Chemchemi zilizoko katika eneo hili, pamoja na chemchemi ya Kaisaria Filipi, ndivyo vyanzo vikuu vya Mto Yordani. Kiwanja cha hekalu la Yeroboamu kimepigwa picha hapa.

Matukio Muhimu: Ibrahimu alimwokoa Lutu (Mwa. 14:13–16). Kabila la Dani liliteka eneo hili na kuliita Dani (Yos. 19:47–48). Yeroboamu alitengeneza hekalu la uongo na ndama wa dhahabu ambavyo vilichangia anguko la makabila kumi ya kaskazini (1 Fal. 12:26–33). Dani ulikuwa mji wa Israeli uliokuwa kaskazini ya mbali kabisa—kuanzia hapa maandiko huitaja nchi ya Israeli “kuanzia Beer-sheba hata kwa Dani” (2 Nya. 30:5; Beer-sheba ulikuwa mji wa kusini ya mbali kabisa). (Ona MWM Dani.)