Misaada ya Kujifunza
4. Kadeshi-barnea


4. Kadeshi-barnea

Picha
picha 4

Huu ni uelekeo wa kaskazini mashariki ya bonde kuu la jangwa (pia huitwa korongoni) hapa ndipo Kadeshi-barnea ilipo. Kijito kinachotiririka hapa wakati wa majira ya mvua hupafanya hapa kuwa mahali panapomwagiliwa vyema na mahali panapozalisha katika nyika ya Zini.

Matukio Muhimu: Hapa yawezekana kuwa ndipo mahali ambapo Musa aliwatuma wanaume 12 kwenda kuipeleleza nchi ya Kaanani (Hes. 13:17–30). Ilitumika kama kituo muhimu kwa Waisraeli katika miaka 38 kati ya karibu miaka yao 40 ya kutangatanga nyikani (Kum. 2:14). Miriamu akafa na kuzikwa hapa (Hes. 20:1). Hili lilikuwa ndilo eneo la uasi wa Kora, manungʼuniko ya watu, na kuchipuka kwa fimbo ya Haruni (Hes. 16–17) karibu na hapa Musa alipiga mwamba na maji yakatoka (Hes. 20:7–11).