Misaada ya Kujifunza
29. Athene


29. Athene

Picha
picha 29

Picha hii, iliyopigwa kutoka Arepago (Kilima cha Marsi) inaonyesha Akropolo ya Athene, eneo la madhabahu kwa miungu kadha wa kadha wa kipagani Athene ulikuwa ndiyo mji mkuu wa kale wa Uyunani ya Atika na katika nyakati za Agano Jipya ulikuwa katika jimbo la Kirumi la Akaya. Uliitwa kwa heshima ya jina la mungu mwanamke wa kipagani wa Wayunani Athena. Kwa nyakati za Agano Jipya, Athene ilikuwa imepoteza sehemu kubwa ya ukuu na utukufu wake wa awali, lakini bado ulikuwa na sanamu na minara ya kumbukumbu za miungu wengi wa kiume na wa kike, ikiwa ni pamoja na “Mungu Asiyejulikana” (Mdo. 17:23).

Matukio Muhimu: Mtume Paulo aliutembelea mji huu na akahubiri mahubiri yake juu ya “Mungu Asiyejulikana” juu ya Kilima Marsi (Mdo. 17:15–34). Wamisionari walitumwa kutoka Athene kwenda sehemu nyingine za Uyunani (1 The. 3:1–2).