Misaada ya Kujifunza
19. Kaisaria na Uwanda wa Sharoni hadi Karmeli


19. Kaisaria na Uwanda wa Sharoni hadi Karmeli

Picha
picha 19

Ukiangalia kuelekea Kaskazini ngʼambo ya bandari ya kale ya Kaisaria na Uwanda wa Sharoni. Pia katika mandhari juu ya picha ni safu ya milima ya Karmeli.

Matukio Muhimu: Eliya alipambana na makuhani wa uongo wa Baali katika Mlima Karmeli (1 Fal. 18). Via Maris (Njia ya Bahari), ni barabara muhimu katika nyakati za Kale, ilikuwa mashariki ya Kaisaria. Baada ya ono la kustaajabisha wakati akiwa Yafa, Petro alianza huduma miongoni mwa Wayunani kwa kumfundisha akida wa Kirumi aliyeitwa Kornelio katika Kaisaria (Mdo. 10). Filipo aliishi na kufundisha hapa na alikuwa na mabinti watatu waliokuwa wakitoa unabii (Mdo. 8:40; 21:8–9). Paulo alikuwa mfungwa gerezani katika mji huu kwa miaka miwili (Mdo. 23–26). Aliwahubiria Felix, Festo, na Herode Agripa Ⅱ, ambaye alisema, “Karibu ungenishawishi kuwa Mkristo” (Mdo. 26:28).