Misaada ya Kujifunza
10. Ngazi za Kwenda Hekaluni


10. Ngazi za Kwenda Hekaluni

Picha
picha 10

Eneo la hekalu liligawanywa katika mabaraza, na mabaraza ya nje yalisimama kwenye kiwanja kilichokuwa chini zaidi. Wafanya ibada waliingia kupitia milango mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ile iliyoelekea upande wa juu kutoka ngazi hizi kuingia katika mabaraza ya nje na halafu ndani ya mabaraza yaliyo ndani zaidi. Maelfu ya watu wamepanda ngazi hizi kwa muda mwingi, ikiwa pamoja na Mwana wa Mungu. Wakati majeshi ya Tito yalipoliangamiza hekalu katika mwaka 70 B.K. ngazi hizi zilifunikwa kwa kifusi. Zilifukuliwa na wanaakiolojia katika miaka ya 1970 wakati wa uchimbaji wa sehemu ya mji wa zamani wa Yerusalemu.

Tukio Muhimu: Ezekieli aliona katika ono ukubwa na aina ya hekalu la wakati wa baadaye (Eze. 40). (Ona MWM Hekalu, Nyumba ya Bwana.)