Misaada ya Kujifunza
17. Shekemu


17. Shekemu

Picha
picha 17

Ni eneo la zamani la Shekemu Katika sehemu ya mbele ya picha ni Mlima Gerizimu, na ngʼambo yake, ni Mlima Ebali. Shekemu iko katikati ya milima hii miwili.

Matukio Muhimu: Ibrahimu alipiga kambi katika Shekemu (Mwa. 12:6–7). Yakobo alipiga kambi hapa na akanunua sehemu ya ardhi (Mwa. 33:18–20). Mlima Gerizimu ulikuwa ni mlima wa baraka, wakati mlima Ebali ulikuwa ni mlima wa laana (Kum. 27–28). Katika Mlima Ebali, Yoshua alijenga mnara wa ukumbusho uliokuwa na torati ya Musa na kisha akasoma torati hiyo kwa Waisraeli (Yos. 8:30–35). Mifupa ya Yusufu imezikwa katika Shekemu (Yos. 24:32).