Misaada ya Kujifunza
6. Nchi ya Milima ya Uyahudi


6. Nchi ya Milima ya Uyahudi

Picha
picha 6

Nchi ya milima ya Uyahudi ni karibu kilomita 56 urefu na kilomita 27 upana. Sehemu kubwa ya nchi ni mawe mawe na ni vigumu kuilima. Milima inagagwanywa kwa mabonde ambayo ndiyo ardhi nzuri yenye kuzalisha. Waisraeli wa awali waliishi katika milima hii, na waliitumia kwa ulinzi dhidi ya wavamizi.

Matukio Muhimu: Bwana aliahidi nchi hii kwa Ibrahimu na uzao wake (Mwa. 13:14–18; 17:8). Sara na Ibrahimu walizikwa katika pango la Makpela, katika Hebroni (Mwa. 23:19; 25:9). Daudi aliiteka Yerusalemu kutoka Wayebusi (2 Sam. 5:4–9). Matukio mengi zaidi ya Agano la Kale yameandikwa kama yametokea katika milima hii kuliko katika eneo lingine lolote.