Rafiki
Mkufu Ung’aao
Ubatizo na Uthibitisho


“Mkufu Ung’aao,” Rafiki, Agosti 2023, 42–43.

Mkufu Ung’aao

Carolina alitaka tu kuwa na mkufu kwa muda kidogo.

Hadithi hii ilitokea huko Ajentina.

Picha
alt text

Carolina aliruruka ua. Rafiki yake Isabella alikuwa nje.

Isabella alipunga mkono. “Njoo tucheze!”

Carolina alivuka ua hadi nyumbani kwao Isabella.

Isabella aliingiza mkono mfukoni. “Ninataka kukuonyesha kitu,” alisema. Kisha akatoa mkufu uliokuwa mzuri sana ambao Carolina hakuwahi kuuona! Vito hivi vidogo vilikuwa vinang’aa na ni angavu.

“Ni vya mama yangu,” Isabella alisema. “Alisema ningeweza kucheza navyo leo. Vitazame juani.”

Isabella aliushikilia mkufu katika mwanga. Mamia ya pinde za mvua ziliakisi kwenye vito. Ilikuwa ya kupendeza sana!

“Sasa acha tucheze kujificha na kutafutana!” Isabella alisema.

“SAWA!” alisema Carolina. “Ninaweza kusaidia kuuweka mkufu salama.”

“Asante!” Isabella akampa Carolina mkufu, na Carolina akauweka mfukoni mwake.

Punde ikawa wakati wa Carolina kwenda nyumbani. Aliposema kwaheri, Isabella hakumuuliza kuhusu mkufu. Lazima alikuwa amesahau. Na Carolina hakumkumbusha.

Carolina alihisi vibaya kidogo kwa kwenda na mkufu nyumbani. Lakini alikuwa anataka kuwa na mkufu kwa muda kidogo tu. Alipuuza hisia mbaya na kuuweka mkufu chini ya mto wake.

Siku iliyofuata ilikuwa Jumamosi. Carolina alifanya kazi zake na kwenda nje kucheza. Alisahau kabisa kuhusu mkufu.

“Carolina!” Baba aliita. Unaweza kuja hapa?”

Carolina alikimbia ndani. “Ndiyo!”

Baba aliushikilia mkufu katika mkono wake. Mama ameupata chini ya mto wako. Ni wa nani?

“Ni wa Isabella.” Machozi yalilengalenga katika macho ya Carolina. “Nikuwa nimeuweka salama katika mfuko wangu tulipookuwa tunacheza jana. Lakini kisha niliamua kuuleta nyumbani.

Mama alikaa na Carolina kwenye kochi. “Asante kwa kusema ukweli. Unadhani tunapaswa kufanya nini sasa?

Carolina alikuwa kimya. Akafikiria kuhusu Yesu. Angemtaka yeye kuwa mwaminifu na kurudisha mkufu.

“Ninapaswa kumrudishia Isabella na kumwambia samahani,” Carolina alisema. Punde aliposema hivyo, hisia mbaya ziliondoka. Alihisi vizuri moyoni.

Carolina alienda nyumbani kwa Isabella.

“Mambo,” Carolina alisema. Akamrudishia Isabella mkufu. “Samahani niliuchukua. Utanisamehe?”

“Ndiyo,” Isabella alisema. “Asante kwa kuurudisha.” Kisha akatabasamu. “Unataka tucheze kujificha na kutafutana?”

“Ndiyo! Hesabu kwanza—mimi nitaenda kujificha!”

Usiku ule, Carolina alisali. “Baba wa Mbinguni mpendwa, tafadhali nisamehe kwa kuchukua mkufu ule. Nakushukuru Wewe kwa kunisaidia kusahihisha hilo.”

Carolina alihisi hisia za ukunjufu tena. Alikuwa na furaha kwamba angeweza kufanya kile ambacho Yesu angependa yeye afanye.

Picha
alt text
Picha
alt text here

Vielelezo na Sue Teodoro