Rafiki
Jinsi Nilivyobatizwa
Ubatizo na Uthibitisho


“Jinsi Nilivyobatizwa,” Rafiki, Agosti 2023, 12–13.

Jinsi Nilivyobatizwa

Picha
alt text

Mambo! Mimi ni Aranoarii. Ninaishi Tahiti. Mimi nina umri wa miaka 11, na ninahisi fahari kusema kwamba mimi ni muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Ni kwa jinisi gani ulijifunza kuhusu Kanisa?

Picha
alt text
Picha
alt text

Marafiki fulani waliialika familia yangu kwenye shughuli ya Kanisa. Sisi pia tulialikwa kwenye ubatizo wa mtoto. Nilimuuliza mama yangu kama ningeweza kukutana na wamisionari kwa sababu kweli nilitaka kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo.

Ilikuwa vipi kukutana na wamisionari?

Picha
alt text

Wamisionari walikuwa wakarimu kweli! Mimi daima nilisisimka kuwa na masomo na wao kumhusu Yesu Kristo na injili Yake. Nilipendelea hadithi walizonisimulia na michezo tuliyocheza ili inisaidie kujifunza.

Ubatizo wako ulikuwaje?

Picha
alt text

Baba yangu alimbatiza mama yangu pamoja na mimi kwenye siku yangu ya kutimiza miaka 11 ya kuzaliwa. Nilikuwa mwenye furaha sana! Tuliwaalika watu wengi ambao tunawapenda. Wanafunzi wenzangu na mwalimu walikuja kuniunga mkono.

Nilipotoka majini, nilijawa na shangwe. Nilitabasamu kabisa! Nilikuwa na furaha sana kwamba niliweza kufuata mfano wa Yesu Kristo.

Je, ilikuwaje kwenda kwenye Msingi kwa mara ya kwanza?

Picha
alt text

Mwanzoni, nilikuwa na wasiwasi nilikuwa karibu kulia. Lakini kisha nilienda kwenye shughuli ya Msingi. Nilipata kumjua kila mtu, na nikapata marafiki kadhaa.

Kama wewe ni mgeni, ushauri wangu ni njoo kwenye darasa lako la Msingi, hata kama unaogopa mwanzoni. Tunawapenda wageni!

Je, ni kwa jinsi gani wewe unamfuata Yesu?

Picha
alt text

Ninasali na kwenda kanisani kila Jumapili. Ninazungumza na familia yangu kuhusu injili ya Yesu Kristo.

Ninajaribu kuwajali wengine ambao wanahitaji msaada. Nyumbani, ninamsaidia mama yangu kazi za nyumbani. Ninamsaidia baba yangu kazi za shamba, kukata kuni, na kujenga vitu. Miezi michache iliyopita kata yetu ilikuwa na maonyesho ya vipaji. Mimi ni mwanamuziki, kwa hiyo nilipiga ngoma usiku mzima!

Picha
alt text here

Picha na Stéphane Sayeb