Rafiki
Sala ni Nini?
Ubatizo na Uthibitisho


“Ni kwa Jinsi Gani Tunasali? Rafiki, Agosti 2023, 24.

Ni kwa Jinsi Gani Tunasali?

Picha
alt text

Sala ni jinsi sisi tunavyozungumza na Baba wa Mbinguni. Yeye daima anataka kusikia kutoka kwako, Yeye daima husikiliza. Yeye hujibu sala zetu katika njia nyingi. Yeye anaweza kukupa mnong’ono, au hisia, kutoka kwa Roho Mtakatifu. Au Yeye anaweza kumpa mtu mwingine msukumo akusaidie wewe.

Jinsi ya Kusali

  • Funga macho yako, inamisha kichwa chako, na ukunje mikono yako.

  • Anza kwa kusema, “Baba Mpendwa wa Mbinguni.”

  • Zungumza na Baba wa Mbinguni kwa heshima na staha.

  • Malizia kwa kusema, “Katika jina la Yesu Kristo, amina.”

  • Unaweza kusali kwa kupaza sauti au katika akili yako, wakati wowote.

Hapa kuna baadhi ya mambo unayoweza kusali kuyahusu:

  • Kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya mambo uliyo na shukrani kwayo.

  • Kumwambia Yeye kuhusu mambo magumu au rahisi ambayo yalitendeka katika siku yako.

  • Kumwomba msaada wakati unaogopa au hujui nini cha kufanya.

  • Kumwomba Yeye ambariki mtu mwingine ambaye anahitaji msaada.

Ninakushukuru . . .

Picha
alt text here