Rafiki
Agano Langu la Ubatizo
Ubatizo na Uthibitisho


“Agano Langu la Ubatizo,” Rafiki, Agosti 2023, 10–11.

Agano Langu la Ubatizo

Agano ni ahadi tunayofanya na Baba wa Mbinguni. Soma kuhusu vitu vitatu tunavyoahidi kufanya tunapobatizwa. Kisha andika kuhusu kile unachoweza kufanya ili kushika agano lako la ubatizo.

Daima Kumkumbuka Yesu Kristo

Picha
alt text

“Daima kumkumbuka yeye” (Moroni 4:3).

Wakati Elena alipowaona wengine wakimtendea mabaya mtu fulani, alifikiria kile ambacho Yesu angefanya.

Je, ninawezaje kumkumbuka Yesu: _____________

Kushika Amri Zake

Picha
alt text

“Kushika Amri Zake” (Moroni 4:3).

James alichagua kutoangalia video zilizo na maneno na picha mbaya.

Amri Ninayoweza kushika: _____________

Jichukulie Jina Lake Juu Yako

Picha
alt text

“Jichukulie juu [yako] jina la [Yesu Kristo]” (Moroni 4:3).

Nana alimwambia rafiki yake kwamba yeye ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Kile ambacho kujichukulia jina Lake juu yetu humaanisha kwangu: _____________

Kushika Agano Langu

Hapa kuna baadhi ya njia za kushika agano lako la ubatizo.

Wasaidie Watu

Picha
alt text

“Kubebeana mizigo, ili ipate kuwa miepesi” (Mosia 18:8).

Akio alimsaidia mdogo wake kazi yake ya nyumbani ya hisabati.

Nani ninaweza kumsaidia: ___________

Tubu Unapofanya Kosa

Picha
alt text

“Watubu na kuzaliwa tena” (Alma 5:49).

Baada ya Isa kusema kitu kibaya kwa dada yake, aliomba kwa Baba wa Mbinguni. Kisha alimuomba dada yake amsamehe.

Jinsi gani ninaweza kutubu: ___________

Wafariji Wengine

Picha
alt text

“Kufariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa” (Mosia 18:9).

Lucas alimtembelea rafiki yake ambaye babu yake amefariki.

Jinsi gani ninaweza kumfariji mtu: ____________

Picha
alt text here

Vielelezo na Kelly Smith