Rafiki
Kumsikia Roho Mtakatifu
Ubatizo na Uthibitisho


“Kumsikia Roho Mtakatifu,” Rafiki, Agosti 2023, 21.

Kumsikia Roho Mtakatifu

Picha
Alt text

Kielelezo na Xavier Bonet

Msimu wa joto uliopita, familia yangu ilienda safari ya kupanda mlima. Njia iliongoza kwenye kijito. Dada yangu, kaka mdogo wangu, na mimi tulivua viatu vyetu na kutembea ndani ya maji.

Wakati maji yalipovuka magoti yangu, tulisimama. Tuliona kundi la watoto wakubwa wakicheza ndani ya maji yenye kina kirefu mbele yetu. Dada yangu alitabasamu na kusema, “Twendeni mbali zaidi!.”

Lakini sauti akilini mwangu iliniambia nibaki nyuma pamoja na mdogo wangu. Nilijua alikuwa ni Roho Mtakatifu. Nilimwambia dada yangu kwamba angeweza kwenda kuangalia, lakini mimi na mdogo wangu tungebakia.

Wakati dada yangu aliporudi, alisema maji yalikuwa na mkondo mkali na ilikuwa vigumu kutembea ndani yake. Aliposema hivyo, nilijua nilikuwa nimefanya chaguo sahihi kubakia salama pamoja na mdogo wangu.