Rafiki
Ninaweza Kumfuata Yesu Kristo
Ubatizo na Uthibitisho


“Ninaweza Kumfuata Yesu Kristo,” Rafiki, Agosti 2023, 40–41.

Ninaweza Kumfuata Yesu Kristo.

Picha
alt text

Yesu aliwatumikia wengine (ona Yohana 13:5, 13–17). Ninaweza kuona kile watu wanachohitaji na kufanya vyema kadiri niwezavyo ili kusaidia.

Picha
alt text

Yesu aliwajumuisha wengine (ona Marko 10:14). Ninaweza kuwajumuisha wengine na kuwa rafiki kwa wale ambao wanahisi kutengwa.

Picha
alt text

Yesu alisali kwa ajili ya wengine (ona 3 Nefi 17:15–18). Ninaweza kuzungumza na Baba wa Mbinguni kupitia sala. Ninaweza kumwomba Yeye awabariki wengine pia.

Picha
alt text

Yesu aliwasamehe wengine (ona Yohana 8:11). Ninaweza kuwasamehe wengine pia. Wakati ninapofanya uchaguzi usio sahihi, ninaweza kusema, “Samahani.”

Picha
alt text

Yesu alifundisha injili (ona Mathayo 5:1–9). Ninaweza kushiriki injili pamoja na wengine. Ninaweza kuwafundisha watu wengine kuhusu Yesu.

Picha
alt text

Yesu aliweka mfano mkamilifu (ona Yohana 13:15). Ninaweza kufanya vyema zaidi katika kumfuata Yesu. Ninaweza kuwa mfano kwa wengine pia.

Picha
alt text here

Vielelezo na Olga Lee