Rafiki
Rafiki Zetu Wadogo Wapendwa,
Ubatizo na Uthibitisho


“Rafiki Zetu Wadogo Wapendwa,” Rafiki, Agosti 2023, 1.

Rafiki Zetu Wadogo Wapendwa,

Picha
alt text

Tunatumaini utaweza kufurahia hili toleo maalumu la Rafiki. Ni yote kuhusu kubatizwa na kuthibitishwa.

Kama umebatizwa karibuni, tunakukaribisha wewe kama muumini mpya wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho!

Unapobatizwa, unafuata mfano wa Mwokozi wetu,Yesu Kristo. Wewe unaahidi kumkumbuka Mwokozi na kutii amri Zake. Ahadi hizi zinaitwa maagano. Unapothibitishwa, unapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kisha Roho Mtakatifu anaweza kukufariji, kukuongoza na kukupa mwongozo wa kiungu kote maishani mwako.

Kama tayari umebatizwa, tunakuhimiza ukumbuke agano ulilofanya ulipobatizwa na kujaribu kumfuata Yesu kila siku.

Kama hujabatizwa bado, tunatumaini utajiandaa kwa kujifunza zaidi kuhusu hatua hii muhimu.

Tunaona fahari kubwa juu ya kila mmoja wenu. Tunajua kwamba Baba wa Mbinguni anawalinda ninyi. Yeye anawapenda ninyi sana, na sisi vivyo hivyo.

Urais wa Kwanza

Picha
alt text
Picha
alt text here