Rafiki
Siku Kubwa ya Giorgia
Ubatizo na Uthibitisho


“Siku Kubwa ya Giorgia,” Rafiki, Agosti 2023, 8–9.

Siku Kubwa ya Giorgia

“Nitabatizwa hivi karibuni,” alisema. “Kama tu Yesu alivyobatizwa!

Hadithi hii ilitokea huko Australia.

Picha
alt text

Giorgia alikimbia hadi chumbani kwake pamoja na Matilda akiwa karibu kwa nyuma. Daima ilikuwa siku ya burudani wakati rafiki alipokuja kucheza naye.

“Je, tunaweza kucheza na roboti yako? Matilda aliuliza.

“Ndiyo!” Giorgia alisema. Ilikuwa mojawapo ya vitu alivyopenda kufanya.

Wakati Giorgia akitoa roboti, Matilda alitazama picha kwenye ukuta wa Giorgia. Aliionyesha picha iliyokuwa katikati.

“Hiyo ni nini?” aliuliza.

“Huyo ni Yesu Kristo akibatizwa,” Giorgia alisema. “Na mimi nitabatizwa hivi karibuni. Kama vile Yeye alivyobatizwa!”

Kwa nini unabatizwa? Matilda aliuliza.

“Kwa sababu ninataka kumfuata Yesu.” “Ninapobatizwa, hicho ndicho nitaahidi kufanya!”

Kisha Matilda akapata wazo. “Je, ungependa kuja kwenye ubatizo wangu?”

“Nitamuuliza mama yangu ikiwa ninaweza,” Matilda alisema.

Siku ya ubatizo wa Giorgia ilizidi kusonga karibu. Alisoma kutoka kwenye kitabu chake hadithi za maandiko na alienda katika darasa la Msingi kila wiki. Baada ya kusema maombi yake ya wakati wa kulala, aliitazama picha ya Yesu. Alipenda kufikiria kubatizwa kungekuwaje.

Jumapili kabla ya ubatizo wake, Giorgia alikuwa na usaili wa ubatizo. Yeye na wazazi wake walizungumza na askofu ofisini kwake. Askofu alimuuliza baadhi ya maswali kusaidia kuhakikisha kwamba alikuwa tayari kubatizwa.

Picha
alt text

“Je, Unaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu? aliuliza.

Ndiyo aliamini! “Ndiyo,” alisema.

Askofu alitabasamu. “Ubatizo ni uchaguzi muhimu sana. Je, unataka kubatizwa?”

Giorgia alifikria kuhusu jinsi alivyompenda Yesu na sasa alitaka kumfuata. “Ndiyo!,” alisema.

Hatimaye, siku kubwa ya Giorgia ilifika. Alipoingia ndani ya maji, aliwaona rafiki zake na familia yake wakitazama. Matilda alikuwa hapo pia!

Wakati baba aliposema sala ya ubatizo, maneno hayo yalimfanya Giorgia kuhisi amani na furaha ndani yake. Kisha kwa uangalifu akamtumbukiza moja kwa moja ndani ya maji, na kumtoa nje tena. Alipotoka juu, alihisi kuwa mwenye furaha na msafi.

Baba alimpa Giorgia kumbatio kubwa. Mama alikuwa anamsubiri juu ya ngazi akiwa na taulo na tabasamu.

Giorgia alijisikia vizuri moyoni. Ilikuwa siku maalumu. Alichagua kumfuata Yesu. Na alitaka kuendelea kumfuata kila siku!

Picha
alt text
Picha
alt text here

Vielelezo na Shana Keegan